![]() |
Jupp Heynckes |
Winga
machachari wa klabu ya Bayern Munich,
Franck Ribery ameonyesha furaha yake baada ya klabu yake kuifunga VfB Stuttgart kwa mabao 3-2 katika fainali ya
DFB-Pokal na kuweka historia ya kuwa klabu ya kwanza nchini Ujerumani kushinda
mataji matatu kwa mkupuo.
Winga
huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema kuwa anajisikia furaha na mafanikio hayo
ya kihistoria waliyopata ni kutokana na juhudi pamoja na malengo
waliyojiwekea.
Ribery
aliwashukuru wachezaji wenzake pamoja na mashabiki ambao wamekuwa nao katika
kipindi chote na kuahidi kuwa ataendelea kuwepo klabuni hapo kwa kipindi kirefu
kijacho.
Naye
nahodha wa klabu hiyo Philipp Lahm aliongeza kuwa juhudi zao za ndani na nje ya
uwanja ndizo zilizowafikisha hapo.
Bayern
walifanikiwa kuweka kibindoni taji la Ligi Kuu ya Ujerumani mapema mwezi
uliopita kabla wiki moja baada ya
kuifunga Borussia Dortmund katika Champions League pale Wembley, waliingia kwenye fainali ya DFB
Pokal wakijiamini vilivyo na wakaongoza
mchezo huo kwa mabao 3-0 kabla Stuttgart kufunga mabao mawili ndani ya dakika
10 za mwisho wa mchezo huo.
Hii hapa ndio listi ya vilabu vya UEFA ambavyo vimewahi kubeba makombe matatu ndani ya msimu mmoja (kombe la ligi, kombe la Fa, na Kombe la ulaya):-
Bayern Munich (Germany) 2012/2013.
Inter Milan (Italy) 2009/2010.
FC Barcelona (Spain) 2008/2009.
Manchester United (England) 1998/1999.
PSV Eindhoven (Netherlands) 1987/1988.
Ajax (Netherlands) 1971/1972.
Celtic (Scotland) 1966/1967.
Hiyo
ilikuwa Mechi ya mwisho kwa Kocha wa Bayern Jupp Heynckes ambae anastaafu na
nafasi yake kuchukuliwa na aliekuwa Kocha wa FC Barcelona Pep Guardiola.
Mbali
ya Bao 2 za Mario Gomez, Bao la kwanza la Bayern lilifungwa na Penati ya Thomas
Mueller.
Bao
za Stuttgart zilifungwa na Martin Harnick.
Huu
ni ushindi wa 15 katika Mechi 16 walizocheza mwisho Bayern Munich na kipigo
chao cha mwisho walikipata Oktoba Mwaka jana.
No comments:
Post a Comment