Bernand Membe |
Serikali
imesema italiangalia upya suala la vilabu vya soka vya Tanzania vya Simba,
Yanga na Falcon kwenda nchini Sudan kushiriki katika michuano ya Kombe la
Kagame ambayo inaandaliwa na Baraza la Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na
Kati-CECAFA.
Hatua hiyo
imefikiwa baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernand
Membe kuulizwa juu ya usalama wa timu hizo zitakapokwenda jijini Darfur ambako
michuano hiyo imeandaliwa.
Membe
amesema mpaka sasa hali ya kiusalama katika mji huo bado haijakaa vizuri kwani
wageni wote wanaofika huko hupokelewa kwa magari maalumu ya kuzuia risasi
pamoja na nguo ngumu za kuzuia risasi.
Waziri huyo
aliendelea kusema kuwa pia hakuna hoteli nzuri na zenye usalama na kuonyesha
kushangazwa na watu waliokubali michuano hiyo ifanyike huko wakati wanajua hali
ya kiusalama sio shwari.
Membe amesema kama wizara kwa kushirikiana na
vyombo vinavyohusika vitatoa taarifa za awali kabla ya hawajatoa mapendekezo
kinyume chake ili kuzuia uwezekano wa kuzitosa timu zetu sehemu ambayo inaweza
kuhatarisha usalama wao.
Michuano ya Kagame safari hii imepangwa
kufanyika katika miji ya Darfur ya Kaskazini pamoja na Gordofan ya Kusini
Kuanzia Juni 18 mpaka Julai 2 mwaka huu ambapo kutakuwa na makundi matatu huku
Kundi A likiwa na timu za Merreikh-Elfasher ya Sudan, APR ya Rwanda, Simba ya
Tanzania na Elman ya Somalia.
Wakati kundi
B litakuwa na timu za Al-Hilal-Kaduugle ya Sudan, Tusker ya Kenya, Al Nasir ya
Sudan Kusini, Falcon ya Zanzibar na Al Ahly Shandi ya Sudan huku kundi C likiwa
na timu za Yanga ya Tanzania, Express ya Uganda, Ports ya Djibouti na Vital O
ya Burundi.
No comments:
Post a Comment