Albert Mangweha. |
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii
wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangweha, aliyefariki huko
Afrika Kusini katika hospitali ya St.
Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne
tarehe 28 Mei, 2013.
Kifo cha
Albert Mangweha ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa.
Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan
aina yake ya uimbaji ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana
ndani na nje ya nchi.
Albert
Mangweha atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki
hapa nchini.
Serikali
inawapa pole ndugu na jamaa wote na
kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.
Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
“Mwenyenzi
Mungu ailaze roho ya Albert Mangweha mahala pema peponi.”
Imetolewa na
Waziri wa Habari
Vijana Utamaduni na Michezo
Dkt Fenella
Mukangara.
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI.
Kamati ya
msiba tunaomba kutoa ya taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert Mangweha
hautoweza kufika siku ya Jumapili ya tarehe 2/06/2013 kama ilivyo taarifiwa
hapo awali, hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.
Kwa sasa
tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu waliopo nchini
Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba
radhi Watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu
kwa hili.
Asante
Mwenyekiti
wa Kamati
Kenneth
Mangweha.
Balozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini Radhia Msuya, akiweka saini katika kitabu cha
maombelezo nyumbani kwa baba mdogo wa Marehemu Mangweha Mbezi Beach jijini Dar
leo.
|
Balozi Msuya
akimpa mkono wa pole mama mdogo wa Marehemu Mangweha, Ella Mangweha.
|
Balozi Msuya
(katikati) akibadilishana mawazo na baba mdogo wa marehemu David Mangweha
(kulia) na mama mdogo Ella (kushoto).
|
Balozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya amefika nyumbani kwa mama mdogo wa marehemu
Mangwea Mbezi, Goige jijini Dar es Salaam, leo na kutoa neno.
Akizungumzia
msiba wa Albert Mangwea alisema amesikitishwa sana na kama Mtanzania, amewapa
pole ndugu, jamaa, marafiki na wanamuziki wote nchini.
Akizungumza
katika msiba huo alisema: “Mtu anayefia hospitali na nyumbani ni tofauti,
alitakiwa kufanyiwa uchunguzi, ubalozi unafanyia kazi kibali ambacho
kinatarajiwa kupatikana kesho (Jumatatu), ili ikiwezekana mwili wa marehemu
uwasili hapa nchini Jumanne.
“Taratibu
zinazopitiwa ni za kawaida ila kwa kutokana na umaarufu wa aliyefariki ndiyo
inaonekana hivyo, hata kama ingetokea hapa kwa mtu wa nchi nyingine utaratibu
ungekuwa ni uleule.
“Nitoe wito
kwa vijana kuwa wanapokuja Afrika Kusini wanatakiwa kufuata taratibu na kutoa
taarifa ubalozini, hiyo inarahisisha kutoa msaada pindi kunapotokea tatizo,”
alisema balozi Radhia.
![]() |
Miraji
Kikwete (kushoto) akikabidhi fulana kwa kwa ajili ya shughuli za msiba wa
Mangweha. Katikati ni TID na P-Funk (kulia).
|
![]() |
Miraji akiwa
katika pozi na fulana sawa na ya marehemu Mangweha hapo chini.…
|
![]() |
Marehemu
Albert Kenneth Mangweha enzi za uhai wake.
|
Mdau wa
muziki nchini, Miraji Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya
Kikwete leo amekabidhi fulana kwa ajili ya shughuli ya msiba wa msanii Albert
Kenneth Mangweha katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment