Wageni waalikwa na ndugu za maofisa waliofuzu mafunzo hayo wakiwa kwenye hafla hiyo.
|
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
wakionesha jinsi ya kukabiliana na adui
kwa kutumia singe.
|
Maofisa wa Polisi wakiwa kwenye hafla hiyo.
|
Askari wa Kikosi cha Farasi wakipita katika uwanja wa paredi wakati wa hafla hiyo.
|
Wahitimu hao wakiwa uwanja wa paredi. (Picha habari
na www.mwaibale.blogspot.com)
|
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharibu Bilal akitoka kukagua gwaride la maofisa hao waliohitimu
mafunzo ya uofisa na ukaguzi.
|
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharibu Bilal, akimvika
cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi Alikunda Urio.
|
Gwaride maalumu la maofisa hao likipita mbele ya mgeni rasmi .
|
Wahitimu hao wakila kiapo cha utii.
|
Maofisa wa Polisi wakionesha utalaamu wa kucheza mchezo wa karate wakati wakikabiliana na adui.
|
Mmoja wa askari wa mwanamke wa jeshi hilo
(kulia), akionesha namna ya kukabiliana na adui.
|
Askari hao wakionesha namna ya kukabiliana na adui kwa kutumia
mikono.
|
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
wakionesha jinsi ya kukabiliana na adui
kwa kutumia singe.
|
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
wakionesha namna ya kukabiliana na
wananchi wakati wa vurugu.
|
Makamu wa Rais
wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Dk. Mohammed Gharibu Bilal amesema serikali
haitakuwa tayari kuvunja kiapo chake na kuona amani ya nchi natoweka.
Kauli hiyo aliitoa wakati akifunga mafunzo ya Uofisa na Wakaguzi Wasaidizi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es Salaam leo.
"Serikali haikotayari kuona amani ya nchi ikivurugwa kupitia kundi la aina fulani hivyo ninyi polisi ndio wenye wajibu wa kulinda amani hiyo pamoja na watu na mali zao" alisema Bilal.
Dk.Ghalib Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika ufungaji wa mafunzo hayo alisema hivi sasa nchi yetu imekuwa ikikabiliwa
na matukio ya vurugu zinazotokana na vyanzo mbalimbali.
Alisema baadhi ya vurugu hizo zinasababshwa na
hisia za kiimani,kisiasa na kijiografia ambazo madhara yake ni makubwa na
tayari yameathiri wananchi wengi.
"Wananchi wa Tanzania hawapendi kabisa kuona
nchi hii ikigeuka kuwa ukanda wa vurugu, tena sisi kama Taifa hatuwezi
kunifaika na vurugu zisizoisha"alisema Dk.Bilal.
Alisema jeshi la polisi lilihapa na kusimamia
amani na utulivu nchini hivyo tunaamini kuwa amani hiyo italindwa kutokana na
viapo walivyoapa.
Aliongeza kuwa hivi karibuni kumeibuka baadhi ya
wananchi kwa sababu zao wameanza kubeza na kudharau kazi wanazofanya askari
wetu kibaya zaidi watu hawa wanaota siku moja watashika dola ya nchi yetu ili
waiongoze nchi.
"Siamini macho yangu kama ndoto zao zitatimia
kama wataendelea na tabia hii ya kudharau na kutoeshimu mamlaka tulizojiwekea
wenyewe kwani kazi ya askari si sawa na kufanya siasa kwani kazi ngumu lakini
ni muhimu kuliwekea Taifa katika twasira ya maendeleo"alisema Bilali.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk.Emanuel Nchimbi amesema askari wa tano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa makosa ya kuiba nyaraka
mbalimbali za serikali na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha baada ya kufungua
akaunti kwa kutumia jina la jeshi hilo.
Alisema watu hao tayari wameshakamatwa na muda
wowote watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao kwa kuwa tayari jalada lao
limeshapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali.
Nchimbi alisema kutokana na tuhuma hizo kujitokeza
aliamua kuunda tume ya uchunguzi ili kugundua ni nani anayefanya tuhuma hizo,
tume hiyo ilikuwa inaongozwa na Kamishna Msaidizi wa polisi Advocate Nyombi
kutoka makao makuu ya upepelezi ya makosa ya jinai.
"Sikutaka kufumbia macho suala hilo timu hiyo
ilifanya kazi yake na juni 22 mwaka huu ilitoa majibu na kubaini askari wa
zimamoto wenyewe ndio wanahusika na ubadhilifu ndani ya jeshi la zimamoto
nchini"alisema Nchimbi.
Aliwataja watuhumiwa wanaotuhumiwa kuwa ni Mkaguzi
Msaidizi wa zimamoto Joseph Mwasabeja, Koplo wa zima moto Hashimu Kapamba,
Koplo wa zimamoto Boniface Mbele,Sajini Meja wa Zimamoto Dankan Mwakajinga na
Koplo wa Zimamoto Kenned Kipali ambao wanatoka ndani ya mkoa wa Dar es Salaam
na nje ya mkoa.
Hata hivyo Waziri Nchimbi alisema vitu
walivyopatikana navyo ni pamoja na hati ya akaunti ya benki inayotumika kuibia
serikali,mikanda 82 ya askari wa jeshi la zimamoto na stakabadhi mbalimbali za
malipo zinazotumiwa na jeshi hilo.
Aidha, alisema mtuhumiwa Kapamba alikamatwa na na
stakabadhi za malipo ya serikali (ERVs)ambazo ni za kughushi hati na fomu
mbalimbali za jeshi hilo zinatumika katika ukaguzi wa viwanda na majengo.
Vilevile alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao
mtuhumiwa mmoja ni mtoto wa Kamishina wa pwani,ambaye aliwasiliana naye na
kumtaka amwasilishe mtoto wake ndani ya masaa mawili kwa ajili ya kujieleza
dhidi ya tuhuma hizo.
Hivyo aliwataka maofisa hao wajue kuwa wanakazi
kubwa wanapokwenda kazini na aliwataka wananchi wote watimize wajibu wao kwa
kufuata sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vya namna hii ambavyo vinavunja
heshima yao na jeshi la zimamoto.
No comments:
Post a Comment