Tazama Brazil ilivyoifundisha Soka Uruguay katika Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara kwa bao 2-1 …Usiku huu ni kati ya Mabingwa wa Dunia Hispania na Italia kutafuta mpinzani wa Brazil ambao walitinga Fainali . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 27, 2013

Tazama Brazil ilivyoifundisha Soka Uruguay katika Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara kwa bao 2-1 …Usiku huu ni kati ya Mabingwa wa Dunia Hispania na Italia kutafuta mpinzani wa Brazil ambao walitinga Fainali .


Hapo jana Bao lililofungwa kwa kichwa na Paulinho katika dakika ya 86, limeipeleka Timu ya Taifa ya Brazil hadi fainali ya michuano ya Kombe la Mabara  baada ya kuifunga Uruguay kwa jumla ya mabao 2-1.












Mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil  wakitazama Timu yao ikiwa mwenyeji katika Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara inachezwa huko Estadio Castelao, Mjini Fortaleza Nchini Brazil kati ya Mabingwa wa Dunia Hispania na Italia kutafuta mpinzani wa Brazil ambao jana walitinga Fainali baada ya kuifunga Uruguay Bao 2-1.


Hapo jana (Juni 26,2013) Bao lililofungwa kwa kichwa na Paulinho katika dakika ya 86, limeipeleka Timu ya Taifa ya Brazil hadi fainali ya michuano ya Kombe la Mabara  baada ya kuifunga Uruguay kwa jumla ya mabao 2-1.




Brazil walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 41 kupitia Fred baada ya kazi nzuri ya Neymar lakini Uruguay wakasawazisha katika dakika ya 48 baada ya mabeki wake kufanya makosa na mara moja Cavani akafunga.




Mechi hiyo ilikuwa ni ya vuta nikuvute na Uruguay ndiyo walianza kupata nafasi ya kufunga baada ya mwamuzi kuwapa mkwaju wa penalty baada ya David Luiz kufanya madhambi ndani ya 18.




Lakini mkwaju wa mkongwe Diego Forlan ukaolewa na kila Julio na kufanya ugumu wa mechi uendelee hadi mwisho Brazil walipofanikiwa kuibuka na ushindi.




Na usiku huu(Juni 27,2013) saa nne , Nusu Fainali ya pili ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara inachezwa huko Estadio Castelao, Mjini Fortaleza Nchini Brazil kati ya Mabingwa wa Dunia Hispania na Italia.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad