Wananchi wakiuangalia mnara wa tangi la maji
ulioanguka na kupoteza maisha ya wananchi watatu leo(Juni 02,2013) asubuhi.
|
Mwili wa
mmoja wa marehemu ukishushwa kutoka katika mnara huo.
|
Daktari
bingwa kutoka Cuba anayefanya kazi zake Kisiwani Pemba, (jina halikufahamika)
akimtibu mmoja kati ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Chake Chake
baada ya ajali hiyo.
|
Wananchi
wakiwa katika hospitali ya Chake Chake kuwaona ndugu zao na kutambua miili.
|
Jumla ya
watu watatu wamefariki dunia papo hapo na watatu kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa mnara wa tanki
la maji uliopo Machomanne Chake Chake Pemba, leo(Juni 02,2013) saa tatu asubuhi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Suleiman
Hassan Suleiman, amesema kuwa, merehemu hao walifikwa na mauti wakiwa katika
kazi ya kuteremsha ukuta wa mnara wa tanki la maji ambao walikuwa wameshaukata.
Kamanda
alisema kuwa idadi ya mafundi waliokuwepo kazini hapo walikuwa ni 12 ambapo
watatu wamepoteza maisha papo hapo na watatu kujeruhiwa na kulazwa katika
hospitali ya Chake Chake na wengine sita walikimbia na jeshi la polisi liko
katika utaratibu wa kuwatafuta kwa ajili ya kuelewa hali zao.
Kamanda
Suleiman aliwataja marehemu hao kuwa ni Juma Rashid Juma (35) mkazi wa
Chanjaani, Suleiman Mohammed Abdiadi 'maarufu kama Golo' (55) mkazi wa Kwale na
Salum Muhidini Vuai 'Bandudu' (35) mkazi wa Madungu wote wakazi wa wilaya ya
Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Na majeruhi
katika ajali hiyo ni pamoja na Jackson John (26) mzaliwa wa Iringa na mkazi wa
Msingini, Ali Saleh Ali (35) mkazi wa Michakaeni na Yohana Richard (25) mkazi
wa Machomanne Chake Chake Pemba.
(Habari/Picha:
Abdi Sueliman na Bakari Mussa, Pemba)
No comments:
Post a Comment