Ujenzi wa
hoteli ya kisasa na ya aina yake umanza
ndani ya bonde kubwa linalokadiriwa kuwa na mita 100 kwenda chini. Imepewa jina
la InterContinental Shimao Hotel.
|
Hoteli hiyo
itakuwa katika jimbo la Songjiang nchini humo na inatarajiwa kugharimu pauni
milioni 345 hadi itakapokamilika.
|
Bonde lilivyo
kabla ya kuanza ujenzi….wa ….Hoteli hiyo itakuwa katika jimbo la Songjiang
nchini Nchina na inatarajiwa kugharimu
pauni milioni 345 hadi itakapokamilika.
|
Aidha Mchoro
wa Hotel hiyo umebuniwa na kampuni ya Atkins ambayo asili
yake ni nchini Uingereza na ndani yake kutakuwa na vyumba 380, baadhi yake
vikiwa chini ya maji.
Wakati
sehemu ya maegesho ya magari huwa chini ya hoteli na vyumba vinakuwa juu,
katika InterContinental Shimao Hoteli, maegesho yatakuwa kwenye paa la hoteli hiyo.
Sehemu ya
paa hilo litakuwa ni majani na michezo kama kuruka katika maji na milima
itapewa sehemu kubwa, pia mchezo wa gofu.
InterContinental
Shimao inatarajiwa kuwa imekamilika ifikapo mwaka 2015 na inaelezwa bei
inakadiriwa kuanzia pauni 200 sawa na Sh 520,000 kwa usiku mmoja.
No comments:
Post a Comment