![]() |
|
Mganga mkuu
mkoa wa Iringa, anasema licha ya takwimu kuonesha kuwa asilimia 62 ya
watanzania wana vyoo bora hali halisi haiku hivyo kutokana na watu wengi
kutothamini vyoo wakati wa ujenzi wa nyumba.
|
![]() |
|
“Watu
wanapofanya ujenzi wa makazi yao wanathamini na kutoa kipaumbele kwenye maeneo
mengine ya nyumba na kuacha choo bila uangalifu mkubwa”,
|
Bw.Robert
Salim Mganga mkuu mkoa wa Iringa, anasema
licha ya takwimu kuonesha kuwa asilimia 62 ya watanzania wana vyoo bora hali
halisi haiku hivyo kutokana na watu wengi kutothamini vyoo wakati wa ujenzi wa
nyumba.
Anasema
wananchi wengi wanavyojenga nyumba zao hawatoi kipaumbele katika ujenzi wa vyoo
bora jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya zao na jamii kwa ujumla.
“Watu
wanapofanya ujenzi wa makazi yao wanathamini na kutoa kipaumbele kwenye maeneo
mengine ya nyumba na kuacha choo bila uangalifu mkubwa”, alisema.
Anasema hata shule nyingi za mijini na vijijini hazina
matundu ya vyoo ya kutosha hivyo kusababisha huduma hiyo kuwa ya foleni.
Aliongeza
kuwa katika shule moja yanatakiwa matundu ya vyoo 50 kwa wavulana na 40 kwa
wasichana lakini hali ilivyo ni shule nyingi zimeruhusiwa kuendelea bila
kukidhi vigezo.
Naye
mwakilishi wa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Donald Mshani
anasema shule nyingi zimeruhusiwa kuendelea licha ya kukidhi vigezo kutokana na
uchache wa rasilimali.
Naye Afisa
afya wa mkoa wa Iringa, Didah Haruni anasema kwa takwimu zilizopo inaonesha
kuwa kiwango cha uwepo wa vyoo ni kikubwa lakini bado kuna tatizo la
muingiliano kati ya uchafu na binadamu.
Chanzo:
mjengwablog.







No comments:
Post a Comment