![]() |
| Bwana Fimbo Butallah. |
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya
Balimi Extra leo(Juni 10,2013) imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano
ya ngoma za asili kwa wakazi wa kanda ya ziwa.
Mashindano haya yanafanyika kwa
mwaka wa nane sasa na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa
maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es
Salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bwana Fimbo Butallah
alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni
kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa katika kusherehekea msimu huu wa
mavuno.
Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na kulinda tamaduni zetu
zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa
pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo baina yetu. Amani ni
nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”.
Bwana Fimbo alifafanua kwamba kwa mwaka huu
mashindano ya Ngoma yatahusisha mikoa mitano ya kanda ya ziwa.
Yataanza rasmi
kutimua vumbi Jumamosi hii tarehe 15 June katika mkoa wa Tabora kisha kuelekea
mikoa ya Shinyanga, Kagera, Mwanza na kumalizikia mkoani Mara katika mji wa
Musoma.
Washindi watakaopatikana katika mikoa watashindanishwa kwa pamoja ili
kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda linategemewa
kufanyika jijini Mwanza katikati ya mwezi wa saba.
Tarehe rasmi za mashindano
haya ni kama inavyoonekana hapa chini:-
1. Mkoa wa Tabora; Jumamosi
tarehe 15
June
Uwanja wa Ipuli Mnadani.
2. Mkoa wa Shinyanga; Jumamosi
tarehe 22 June
Viwanja vya wa Shycom.
3. Mkoa wa Kagera; Jumamosi
tarehe 29
June
Viwanja vya Kaitaba.
4. Mkoa wa Mwanza; Jumamosi
tarehe 06
July
Uwanja wa CCM Kirumba.
5. Mkoa wa Musoma; Jumamosi
tarehe 13 July
Bwalo la Magereza.
6. Mashindano ya Kanda; Jumamosi
tarehe 20 July Uwanja wa CCM Kirumba.
Bwana Fimbo alizungumzia pia zawadi za mwaka huu
katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda kwamba Balimi Extra imetenga zaidi ya
shilingi milioni saba kama zawadi.
Mpangilio wa zawadi ni kama inavyoonekana
hapa chini;-
ZAWADI
|
NGAZI YA MKOA
|
NGAZI YA KANDA
|
Mshindi wa Kwanza
|
600,000
|
1,100,000
|
Mshindi wa Pili
|
500,000
|
850,000
|
Mshindi wa Tatu
|
400,000
|
600,000
|
Mshindi wa Nne
|
300,000
|
500,000
|
Mshindi wa Tano hadi wa Kumi kila kikundi
|
150,000
|
250,000
|
Bwana Fimbo alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa
kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi kufurahi kwa pamoja waburudike na ngoma zetu
za asili kutoka sehemu tofauti tofauti.
Aliwashukuru sana wanywaji wa bia ya
Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba waendelee kuitumia kwani ni kupitia
mchango wao ndipo pia Balimi Extra inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili
yao.






No comments:
Post a Comment