![]() |
Mdomo
ukliwa umeathiriwa
na
bakteria kufuatia kutumiwa
kama njia ya
kufanya mapenzi .
|
Saratani
imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana
na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari.
Takwimu
kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya
mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012.
Mkurugenzi
wa Idara ya Kinga Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania
wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya
mapenzi kwa njia ya mdomo. “Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa
na zinaa “ anasema Dk Mwaiselage.
Tafiti
mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani
ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya
hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee.
Matokeo hayo
yanaonyesha kuwa kati ya saratani 509 za mdomo, saratani 242 zilisababishwa na
Virusi vya Human Papiloma ambavyo hutokana na zinaa.
“Ninachojua
mimi ni kuwa Virusi vya HPV husababishwa na magonjwa ya zinaa, hivyo mtu
anayeugua saratani ya aina hiyo, imetokana na zinaa,” anasema Dk Mosha.
Takwimu hizo
ni zile zilizopatikana kwa watu waliokwenda kufanyiwa uchunguzi katika Mkoa wa
Dar es Salaam pekee.
Dk Mosha
anasema kuwa wanaume ndiyo huathiriwa zaidi na saratani ya mdomo ambapo kwa
hapa nchini, asilimia 53 ya wanaume waliofika MNH kwa ajili ya vipimo,
walibainika kuugua saratani hiyo, huku wanawake wakiwa ni asilimia 47.
Utafiti kama
huo ulifanywa pia na Dk Amos Mwakigonja, mkuu wa Idara ya Patholojia katika
Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS).
Dk
Mwakigonja alifanya utafiti wa saratani ya mdomo aina ya Kaposi’s Sarcoma
ambapo wagonjwa 78 walibainika na saratani hiyo kuanzia mwaka 1990 hadi 2003.
“Saratani za mdomo zipo za aina nyingi na zimetofautiana kulingana na
visababishi vyake,” anasema Dk Mwakigonja.
Katika
utafiti wake Dk Mwakigonja alibaini kuwa wanawake wengi walikuwa na saratani ya
mdomo aina ya Kaposi’s Sarcoma kuliko wanaume.
Hata hivyo,
utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 50 ya wanaume walikuwa na saratani ya
mdomo hatari zaidi (systemic) kuliko wanawake ambao ni asilimia 37.
Chanzo:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment