![]() |
|
Lilian
Soti kutoka Mwanga mjini Kigoma Ni Redd's Miss Kigoma 2013,akiibuka Mshindi
katika shindano liliofanyika Juni 09,2013 ndani ya ukumbi wa Kibo Peak.
|
![]() |
|
Redd's
Miss Kigoma 2013, kutoka kushoto ni mshindi namba 3 Happiness Albagost ,kati
kati ni mshindi namba 1 Lilian Soti na kulia ni mshindi namba 2 Faidha Hamisi.
|
![]() |
|
Top
5 ya Redd's Miss Kigoma 2013 ndani ya ukumbi wa Kibo Peak ikiwa ni kati ya Warembo 12
walipambana jana(Juni 09,2013) shindano
kumtafuta Redd’s Miss Kigoma kwa mwaka huu 2013.
|
![]() |
|
Emanuel
J.Matinde na Waratibu wenzake wakifuatilia kwa makini moja ya matukio
yaliyokuwa yakiendelea ndani ya ukumbi wa Kibo Peak kumtafuta Redd's Miss Kigoma
2013.
|
![]() |
|
Wakionekana
ni Warembo 12 ambao walipanda jukwaani (Juni
09,2013) katika Ukumbi wa Kibo Peak mjini hapa katika shindano kumtafuta Redd’s
Miss Kigoma kwa mwaka huu.
|
Aidha
Warembo 12 walipambana jana(Juni 09,2013) katika Ukumbi wa Kibo Peak mjini Kigoma katika
shindano kumtafuta Redd’s Miss Kigoma kwa mwaka huu 2013.
Kwa
Mujibu wa Waratibu wa shindano hilo, mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ameondoka
na Printer kubwa yenye thamani ya shilingi laki 6 na fedha taslimu laki moja na
nusu , sambamba na kushiriki shindano la kumtafuta mrembo wa Kanda ya Kati
litakalofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni.
Mshindi
wa pili wa shindano la kumtafuta mrembo wa Mkoa wa Kigoma 2013, ameondoka na Printer
yenye thamani ya shilingi laki 4 na fedha taslimu laki 1 na kushiriki shindano
la Kanda ya Kati.
Mshindi
wa tatu ameondoka na Microwave yenye thamani ya laki 2 na fedha taslimu elfu 70
pamoja na kushiriki shindano la kumatafuta mrembo wa Kanda ya Kati.
Picha
na Habari Na:E.Johnson-Kigoma.











No comments:
Post a Comment