Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare aachiwa kwa dhamana Kisutu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2013

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare aachiwa kwa dhamana Kisutu.



Wilfred Lwakatare.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  imekubali kumwachia Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare kwa dhamana ya Shilingi 10Milioni  leo(Juni 11,2013).



Lwakatare  anakabiliwa na kesi ya kujaribu kumwekea sumu Dennis Msaki.



Waliomuwekea dhamana Lwakatare ni Madiwani wawili wa Chadema kutoka kata ya Kimara na Sinza.



Madiwani hao wametakiwa kuhudhuria mahakamani kila kesi hiyo itakapotajwa.


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lwakatare akijadiliana jambo ndani ya mahakama na mtuhumiwa mwenzake, Ludovic.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad