 |
Kikosi cha
wachezaji 73 wa michezo mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngara katika
mashindano ya shule za sekondari nchini UMISETA ngazi ya mkoa wa Kagera
,kimerejea salama wilayani Ngara na
ushindi mkubwa katika mashindano hayo
yaliyohitimishwa jana katika
viwanja vya chuo cha ualimu Katoke mjini
Muleba mkoani Kagera.
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Manispaa ya Bukoba ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara ikiingia uwanjani katika maandamano ya Pmaoja kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya
UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera ,Kanali Fabiani Masawe(Mulokozi) akiimba wimbo wa Kuhamasisha Maendeleo mkoa wa Kagera wakati wa ufunguzi wa
UMISETA 2013 kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera ,wa pili kushoto ni Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Froliani Kimoro na Afisa Michezo mkoa wa Kagera Kefa Eliasi.
|
 |
Afisa Michezo mkoa wa Kagera Kefa Elias akitenga mpira ili mgeni rasmi Kanal Fabiani Masawe afungue rasmi Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013) kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera.
|
 |
Timu ya Mchezo wa Soka toka Wilaya ya Karagwe na Bukoba Vijijini wakielekea Jukwaa kuu kukaguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Fabiani Masawe ili kuanza kurusha karata zao katika mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013) kwenye uwanja wa soka wa chuo cha Ualimu Katoke. |
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara Katika mchezo wa Mpira wa pete(Netball) ikiwa Uwanjani katika Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba
mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21
hadi May 23,2013).
|
| |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara Katika mchezo wa Mpira wa pete(Netball) ikiwa Uwanjani katika Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba
mkoani Kagera ,tayari kushiriki Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21
hadi May 23,2013).
|
Kikosi cha
wachezaji 73 wa michezo mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngara katika
mashindano ya shule za sekondari nchini UMISETA ngazi ya mkoa wa Kagera ,kimerejea
salama wilayani Ngara na ushindi mkubwa
katika mashindano hayo yaliyohitimishwa
jana katika viwanja vya chuo cha ualimu
Katoke mjini Muleba mkoani Kagera.
Akipokea
msafara huo leo(May 24,2013) katika
Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara
,mjini Ngara,kwa niaba ya Mkuu wa wilaya
ya Ngara Kostantine Kanyasu,Katibu tawala wa wilaya Tibaijuka Visent
Josephati amewapongeza mashujaa hao kwa
kuipa ushindi wa kishindo wilaya ya
Ngara katika UMISETA ngazi ya mkoa wa
kagera na kuwataka wachezaji kuimarisha nidhamu na mazoezi ili kujiendeleza zaidi kivipaji vyao pamoja na kujitangaza kiajira.
Issa Sama
ambaye ni Mjumbe wa CCM
- NEC Taifa na mdau mkubwa wa michezo hapa wilayani Ngara, licha ya kutoa
usafiri wa kukisafikisha kikosi
hicho kwa siku zote za mashindano ya
UMISETA ,amesema kupata matunda yenye mafanikio lazima viongozi kuwekeza nguvu zao
kwa dhati na kushirikiana kwa pamoja
katika michezo ili kuendeleza
vipaji na kupata mafanikio kama hayo ambayo leo hii yameletwa ni wanafunzi wa shule za sekondari kupitia UMISETA ngazi ya mkoa wa Kagera.
Kwa Upande
wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Joni Shimilimana akizingumza katika mapokezi
hayo ndani ya viwanja vya Halmashauri ya
wilaya ya Ngara ,amesema halmashauri hiyo itaendelea kusaidia juhudi za kuendeleza michezo ili kuzidi kuitangaza wilaya ya Ngara kupitia
sekta hiyo ya michezo.
Nae afisa
elimu wilaya ambaye kimashindano haya ya
UMISETA ni Mwenyekiti Juliasi Nestori
amesema wilaya ya Ngara imetoa wachezaji 28 kati ya 108 wanaounda kikosi
cha UMISETA mkoa wa Kagera ambacho
kimeanza kambi rasim leo na kwamba
wanaimani na wachezaji hao kufanya vema katika mashindano ya kikanda na hata taifa pia.
Awali Afisa Michezo wilaya ya Ngara Said Salumu alitoa matokeo ya jumla ya wilaya hiyo katika mashindano hayo ya umiseta ngazi ya mkoa wa
Kagera ambapo amesema Halimashauri ya wilaya ya Ngara katika mashindano ya
UMISETA ngazi ya mkoa ilikuwa ni Jumla ya wilaya 7 zilizoshiriki katika
mashindano hayo.
Amesema
licha ya kupangwa kundi B lililokuwa ni timu za Wilaya za Bukoba
Vijijini,Karagwe na Ngara huku kundi A
likiwa na Bukoba Manispaa,Biharamulo,Misenye na Muleba ,Wilaya ya Ngara
ikaibuka Bingwa wa Kimkoa katika mchezo wa Mpira wa Kikapu kwa jumla ya Pointi
57 baada ya kuzifunga timu za Wilaya za
Karagwe na Muleba na Kukabidhiwa Cheti cha Ushindi.
Katika
mchezo wa Mpira wa Wavu(Volleyball),Said Salumu amesema wilaya ya Ngara
ilicheza na Wilaya ya Bukoba na kuwafunga seti 2-0,Karagwe seti 2-0 na kuingia
fainali na Wilaya ya Muleba na kufanikiwa kuwafunga seti 2-1 na hivyo
kutangazwa Mabingwa wa mchezo huo Kimkoa.
Aidha kwenye
Mchezo wa Pete(Netball) Wilaya ya Ngara ilizifunga timu za Wilaya ya Bukoba
Vijijini na Karagwe na kuingia fainali dhidi ya wilaya ya Muleba na kufungwa
magoli 19 – 9 na hivyo kuibuka washindi wa Pili Kimkoa.
Katika
Mchezo wa Soka Mabingwa Kimkoa walikuwa
ni Wilaya ya Biharamulo ,wa pili Karagwe,tatu Kimkoa ni Ngara na wa nne Wilaya
ya Misenyi huku Kipa bora kimkoa ni Nechi Mushi kutoka Wilaya ya Ngara.
Matokeo
mengine katika Mbio za mita 1500,Mshindi wa pili kimkoa ni Sauli Semasanga
kutoka Ngara,Mita 100 ni Dalali Mashughulu toka Ngara akiwa ni mshindi wa
Kwanza Kimkoa.
Kuruka chini
,Mshindi wa Kwanza Kimkoa ni Maria Petter toka Ngara huku Kuruka Juu akiwa ni mshindi wa Pili
Kimkoa.
Pia Wilaya
ya Ngara ikaibuka Bingwa Kimkoa katika Mchezo wa Hand ball.
Katika
Mashindano hayo ya UMISETA mkoa wa Kagera wilaya ya Ngara imetoa wachezaji 28
na Walimu 3 kujumuika na Wachezaji wengine 108 kuunda kikosi cha UMISETA mkoa
wa Kagera kitakachoenda kuunda Kikosi cha UMISETA kanda na Mkoa wa Kigoma
ambapo Mchezo wa Handball 9,Volleyball
4,Mpira wa Kikapu 3,Netball 3,Soka 3 na washindi Kimkoa katika Riadha na Miluko.
 |
Timu ya
UMISETA 2013 ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara Katika mchezo wa Mpira wa Soka ikiwa Uwanjani katika Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba
mkoani Kagera , kutafuta nafasi ya kucheza Fainali dhidi ya Biharamulo ambapo ilifungwa bao 1 - o na hivyo kupata nafasi ya kuwania Mshindi wa tatu Kimkoa katika Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21
hadi May 23,2013).
|
 |
Anaepiga Makofi ni Nechi Mushi akichaguliwa kuwa Kipa bora katika ,kuunda Kikosi cha wachezaji 108 wa UMISETA mkoa wa Kagera katika Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21
hadi May 23,2013).
|
 |
Afisa Michezo wilaya ya Ngara Said Salum akitoa taarifa ya Ushiriki ya wilaya hiyo katika Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21
hadi May 23,2013) ndani ya Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara ,ilipopokelewa kishujaa na Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kisiasa (May 24,2013) pembeni yake ni Mwl.Baraka mratibu UMISETA wilaya.
|
 |
Kuanzia
Kushoto ni Afisa Elimu wilaya ya Ngara Julias Nestory, Issa Sama ambaye ni Mjumbe
wa CCM - NEC Taifa na mdau mkubwa
wa michezo hapa wilayani Ngara , Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Ngara Joni Shimilimana, Katibu tawala wa
wilaya Tibaijuka Visent Josephati na Mwenyekiti wa Huduma za Jamii na Diwani wa
Kata ya Mugoma Bw.Rubagola wakipokea taarifa ya ushiriki wa Wilaya ya Ngara
katika Mashindano ya UMISETA Mkoa wa Kagera (May 21 hadi May 23,2013).
|
 |
Katibu
tawala wa wilaya Tibaijuka Visent Josephati
amewapongeza mashujaa hao kwa kuipa ushindi wa kishindo wilaya ya Ngara katika UMISETA ngazi ya mkoa wa kagera na
kuwataka wachezaji kuimarisha nidhamu na mazoezi ili kujiendeleza zaidi kivipaji vyao pamoja na kujitangaza kiajira.
|
 |
Kwa Upande
wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Joni Shimilimana akizingumza katika mapokezi
hayo ndani ya viwanja vya Halmashauri ya
wilaya ya Ngara ,amesema halmashauri hiyo itaendelea kusaidia juhudi za kuendeleza michezo ili kuzidi kuitangaza wilaya ya Ngara kupitia
sekta hiyo ya michezo.
|
 |
Afisa Elimu
wilaya ya Ngara Julias Nestory, amesema wilaya ya Ngara imetoa wachezaji 28
kati ya 108 wanaounda kikosi cha UMISETA
mkoa wa Kagera ambacho kimeanza kambi rasim leo na kwamba wanaimani na wachezaji hao kufanya
vema katika mashindano ya kikanda na
hata taifa pia.
|
 |
Issa Sama
ambaye ni Mjumbe wa CCM
- NEC Taifa na mdau mkubwa wa michezo hapa wilayani Ngaraamesema kupata matunda yenye mafanikio lazima viongozi kuwekeza nguvu zao
kwa dhati na kushirikiana kwa pamoja
katika michezo ili kuendeleza
vipaji na kupata mafanikio
|
No comments:
Post a Comment