Arjen Robben na goli la dhahabu dhidi ya Borussia Dortmund katika Fainali ya UEFA Champions League na Bayern Munich wakiibuka Washindi wa Kombe hili kwa mara ya 5. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 26, 2013

Arjen Robben na goli la dhahabu dhidi ya Borussia Dortmund katika Fainali ya UEFA Champions League na Bayern Munich wakiibuka Washindi wa Kombe hili kwa mara ya 5.


Wachezaji wa Buyern Munich wakishangilia Ubingwa wa  UEFA Champions League 2012/2013 na kuwa Washindi wa Kombe hili kwa mara ya 5.



Arjen Robben received Man of the Match award from Sir Alex Ferguson.


Jürgen Klopp consoles his BVB players after their UEFA Champions League final defeat.


Ilkay Gundogan wa Borussia Dortmund akiifungia timu yake bao la kusawazisha kwa penalti dakika ya 67 ya mchezo.


Mario Mandzukic (9) wa Buyern Munich akiifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 60 ya mchezo huo wa fainali.



Wachezaji wa Buyern Munich wakishangilia bao lao la pili na la ushindi lililofungwa na Arjen Roben dakika ya 89 ya mchezo.


Goli la dakika ya  89 la  Mchezaji toka Uholanzi Arjen Robben limefuta gundu kwake  na Klabu yake ya  Bayern Munich ya Ujerumani katika Fainali za UEFA Champions League, baada ya Bao hilo kuipa ushindi wa magoli  2-1  Bayern dhidi ya wenzao wa Ujerumani  Borussia Dortmund katika Mechi iliyochezwa Uwanja Wembley Stadium Jijini London nchini Uingereza hapo Jumamosi (May 25,2013)Usiku.





Arjen Robben
Bayern walipoteza Fainali mbili za Champions League katika Miaka mitatu iliyopita, ikiwemo kutolewa kwa Mikwaju ya Penati na Chelsea Mwaka jana tena katika Uwanja wao wenyewe Allianz Arena  lakini safari hii waliibuka Washindi wa Kombe hili kwa mara ya 5.




Ni Real Madrid  toka Hispania ni Bingwa wa Champions League  mara 9  na AC Milan ya Italia akiwa ni Bingwa wa Champions League mara 7, ndio wameshinda Kombe hili mara nyingi kupita Bayern Munich.




Mabingwa wengine wa UEFA Champions League ni Liverpool ya Uingereza mara  5, FC Barcelona ya Hispania Mara 4, Ajax ya Uholanzi Mara  4, Inter Milan ya Italia mara  3 na  Manchester United  ya Uingereza mara 3.




Jupp Heynckes
Kwa Kocha wao, Jupp Heynckes, huu ni ushindi mtamu kwa vile anastaafu na nafasi yake kuchukuliwa na aliekuwa Kocha wa FC Barcelona, Pep Guardiola kwa ajili ya Msimu ujao.




Mara baada ya Filimbi ya mwisho kulia, Arjen Robben alitokwa machozi kwani alikuwepo wakati Bayern Munich inapoteza Fainali mbili kwa Inter Milan, Mwaka 2010, na Chelsea, 2012, ambapo alikosa Penati katika Mikwaju ya Penati iliyoipa Chelsea Ubingwa, na vile vile akiwa na Chelsea katika Miaka ya 2005 na 2007 walitolewa kwenye Nusu Fainali ya Mashindano haya na mara zote hizo walikuwa ni Liverpool ndio waliowabwaga.




Mechi hii ilitangaza vyema Soka la Kushambulia la Ujerumani kwani magoli ya Bayern Munich yalifungwa na Mandzukic Dakika ya 60 na Robben dakika ya  89 huku  goli la Borussia Dortmund likifungwa na Mandzukic Dakika ya 68  kwa Mkwaju wa Penati.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad