![]() |
|
Muono wa
jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU)
katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.
|
![]() |
|
Viongoi
mbali mbali wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiwakumbuka waliotangulia mbele
ya haki.
|
![]() |
|
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika
(AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.
|
![]() |
|
Marais
Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu
ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.PICHA NA IKULU.
|
Viongozi wa
bara Afrika wanasherehekea miaka 50 tangu kuundwa kwake hapo tarehe 25 Mei 1963
kwa jina la Umoja wa Nchi Huru za Afrika kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni na
kumaliza utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.
Sherehe za
maadhimisho hayo zinafanyika leo(May 25,2013) mjini Addis Ababa nchini
Ethopia.
Mwenyekiti
wa Umoja huo Waziri Mkuu wa Ethopia Hailemariam Desalegn katika hotuba
ya ufunguzi, amesema sherehe hizo zitatafuta kuwepo kwa bara lisilokuwa na
umaskini na mizozo na Afrika ambayo raia wake wanafurahia hadhi ya kipato cha
kadri.
Umoja wa
Afrika (AU) wa nchi wanachama 54 ulichukua nafasi ya Umoja wa Nchi Huru
za Afrika (OAU) uliyoanzishwa mwaka 1963 katika harakati za mataifa mengi
kujinyakulia uhuru.
Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon,Rais wa Brazil Dilma Rouseff na waziri wa mambo
ya nje wa Marekani John Kerry ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa
waliojumuika na viongozi wa Afrika kusherehekea miaka 50 ya Umoja wa Afrika.
Rais wa
Ufaransa Franswaa Hollande na makamu Waziri Mkuu wa China Wang Yang pia
wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.
Makundi
mbali mbali ya densi yatawatumbuiza wageni waalikwa wapatao 10,000 katika mji
huo mkuu wa Ethopia.
Umoja wa
Afrika unatimiza miaka 50 Tokea mabadiliko ya kidemokrasia katika Rasi ya
Matumaini Mema na kumalizika vita baridi, Umoja huo unatafuta njia za kuwa na
msimamo wake wenyewe.
Unalenga
kuleta ushirikiano wa kikanda, kuondoa vizuizi vya lugha na biashara na
hatimaye siku moja kuleta muungano wa bara zima la Afrika.
Miaka sita
kabla ya hapo, muasisi Nkurumah kutoka kile kilichokuwa kikijulikana kama
koloni la Uingereza "Pwani ya Dhahabu", leo hii Ghana, aliiongoza
nchi hiyo kuwa huru na akawa ndiye baba wa vuguvugu la uzalendo wa Mwafrika
katika kuliongoza jukwaa la mataifa machanga kupambana dhidi ya ukoloni na
ubaguzi wa rangi.
Muongozo
muhimu, ambao ni ule wa kutoingilia mambo ya ndani ya mataifa mengine huru,
ukageuka hatimae kuwa janga kwa Umoja huo, kwani mtindo wa mapinduzi ya
kijseshi wa miaka ya 1960 na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipotokea, viongozi
wa mataiafa ya Afrika walibakaia kimya wakiangalia .
Baada ya
kuupa jina jipya la Umoja wa Afrika (AU) ambao uliundwa 2002 mjini Durban,
Afrika ya Kusini, baada ya kumalizika vita baridi, madhumuni yake yakawa ni
kuleta muungano wa kiuchumi na demokrasaia.
Kiroja cha
mambo katikati ya miaka ya 1990, kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi
aliyejitangaza "Mfalme wa Wafalme" wa Afrika, alilazimisha fikra ya
mtazamo wa Nkrumah wa "Muungano wa Afrika,", ingawa ilikuwa siasa kwa
masilahi ya kisiasa ya Gaddafi kuliko kuwa hatua ya kifalsafa.
Hata hivyo,
mpango wake wa kuwa na jeshi moja, sarafu moja, biashara na kusafiri bila
vizuizi kama ilivyo katika Umoja wa Ulaya ulisababisha mgawanyiko zaidi kuliko
umoja.
Kutokana na
mvutano huo kukazuka kambi mbili na Afrika ya Kusini yenye nguvu kisiasa
ikasimama kumpinga Gaddafi.
"Bila
shaka matokeo kwetu si ya kuridhisha. lakini tunasonga mbele pamoja na nina
hakika siku hadi siku tutafikia karibu lengo la "Muungano wa Afrika."
Alisema
mjumbe wa Gaddafi kwenye Umoja huo, baada ya kuvunjwa moyo na kile alichokiona
ni udhaifu, aliwaambia wajumbe baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika 2009.
Hayati
Gaddafi mara kwa mara alikuwa akitowa matamshi makali kwa waliompinga kwa
kuzingatia kile alichokiona ni mapenzi ya Waafrika wengi kwake.
Hatimaye
Ingawa wazo hilo lilizusha mabishano na kutoa sura ya mgawanyiko miongoni mwa
mataifa, Umoja wa Afrika sasa una waziri wa ndani wa Afrika ya Kusini Nkosazana
Dlamini-Zuma kama Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo, mwana mageuzi
aliyetangaza haraka kwamba anataka kuona unawajibika zaidi.
Halmashauri
hiyo kuu inataka kuendeleza sera ya kuadhibu kwa kusimamisha uanachama na
vikwazo kwa wanaokiuka katiba na muongozo wake.
Mtihani kwa
uwajibikaji na nguvu za kiutendaji za Umoja wa Afrika, kandoni mwa pigo la
ujumbe wake wa AMISOM nchini Somalia, ni mgogoro katika mataifa ya Afrika ya
Magharibi ya Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kwa Maoni
"Leo Afrika ni ya kidemokrasia zaidi kuliko miaka kumi iliyopita ambapo
tulikuwa na serikali chache zilizochaguliwa kidemokrasia.
Lakini hili
halipaswi kutafsiriwa kwamba ni uongozi wa kidemokrasi.
Demokrasia
ni kutambua fikra tafauti, kwani ndiyo msingi wa matatizo ya kisiasa
Afrika."


.jpg)







No comments:
Post a Comment