![]() |
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt.
Emmanuel Nchimbi akitoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu
vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara.
|
![]() |
Spika wa
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiahirisha Bunge kutokana na vurugu
zilizotokea Mkoani Mtwara.
|
![]() |
Waziri wa
Nchi ofis ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na
Uwezeshaji) Merry Nagu akiomba kutengua
kanuni ya Bunge Na. 38 ili kuruhusu suala la vurugu za Mtwara
kujadiliwa Bungeni.
|
![]() |
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Emmanuel Nchimbi (Kushoto) akizungumza na mbunge wa
Kinondoni Mhe. Iddi Azzan nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya bunge
kuahirishwa.
|
![]() |
Waziri wa
Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
akizungumza na baadhi ya Mawaziri na Wabunge ndani ya ukumbi wa Bunge
mara baada ya Spika wa Bunge kuahirisha bunge.
|
![]() |
Kundi la
Waandishi wa Habari wanaoripoti habari
za Bunge wakitoka ndani ya ukumbi huo mara baada ya Spika wa Bunge kuahirisha kikao
cha Bunge.PICHA NA ZAWADI MSALLA-MAELEZO DODOMA
|
![]() |
Moja ya
bango lenye ujumbe "Gesi ibaki au tugawane nchi" picha hii ni ya
maktaba iliyopiwa katika vurugu hivi karibuni juu ya upingaji wa gesi kutoka
Msimbati kwenda Dar es Salaam.
|
![]() |
Mkazi wa
Mtwaa akiwa anatimua mbio huku akiwa na mtoto baada ya kupigwa kwa bomu la
machozi, kazi kweli kweli.
|
![]() |
Nyumba ikiwa
imebomolewa baada ya kuchomwa moto.
|
![]() |
Gari
likiteketea kwa moto
|
![]() |
Barabara
ikiwa imewekwa vizuriwizi wakati wa vurugu hizo na kusababisha huduma
mbalimbali za kijamii kudorola siku ya Mei 22/ 2013.
|
Serikali
iangalie upya namna inavyolitazama suala la Mtwara. Hivi sasa suala hili
linaonekana kiusalama zaidi badala ya kuliona kama suala la kijamii na
maendeleo lenye kuhitaji kujenga imani ya wananchi.
Suala hili
linahitaji muda na heshima kwa wananchi. Ni vema tuache sauti ya wananchi
kusikika na kuzitolea maamuzi sahihi yenye kujenga kuaminiana na kuheshimiana
kati ya dola na wananchi.
![]() |
Zitto Zuberi Kabwe |
Suala la
Mtwara ni zaidi ya gesi asilia. Ni matokeo ya kutengwa kimaendeleo kwa muda
mrefu. Suala la Gesi ni nafasi ya kuunganisha watu wa kusini na Jamhuri ya
Muungano. Tuamue sasa kufanya maamuzi sahihi na kuunganisha Jamhuri yetu au
kukosea na kudharau na kuivunja Jamhuri yetu.
Kama Kuna
mataifa ya kigeni/makampuni binafsi yanahusika na hali ya Mtwara. Serikali
iyataje mataifa hayo na makampuni hayo hadharani na vibaraka wao.Vinginevyo
nadharia hizi zitaonekana ni ni propaganda tu kwa lengo la kufunika kombe
mwanaharamu apite.
Nadharia
zote za kuelezea masuala ya Mtwara zinakimbia suala la msingi ie kutengwa kwa
muda mrefu sana kwa mikoa ya kusini kwenye maendeleo ya nchi.
Ahadi za Rais Ben
Mkapa kuhusu Mtwara Corridor, ahadi za Rais Jakaya Kikwete za 2005 na biashara
ya korosho ni miongoni mwa malalamiko ya muda mrefu ya wananchi wa Mtwara.
Suala hili la msingi lazima lipatiwe majawabu mwafaka kwa maelezo yenye heshima
kwa wananchi badala ya dharau na vijembe dhidi ya raia.
Kuna kukosa
imani kukubwa kwa wananchi dhidi ya Serikali. Suala hili ni pana zaidi na
linasambaa Tanzania nzima. Malalamiko yanaposhawishiwa kihofu tu huleta
matatizo makubwa sana. Hali ya namna hii haijawahi kutokea nchini mwetu.
Kukamata na kufunga viongozi wa wananchi haitosaidia kamwe.
Kutumia
nguvu ya dola kuzima vuguvugu la wananchi sio njia pekee ya kujenga amani.
Makovu ya kutumia nguvu ya dola huchukua muda mrefu sana kupona. Lazima
kubadili mkakati wa kuongoza na kuliweka Taifa sawa.
Zitto Zuberi
Kabwe (Mb)
24th May
2013
No comments:
Post a Comment