Utafiti: Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli endapo uchaguzi mkuu wa Urais 2015 ungefanyika sasa, kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wangekabana koo . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 07, 2013

Utafiti: Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli endapo uchaguzi mkuu wa Urais 2015 ungefanyika sasa, kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wangekabana koo .


Edward Lowassa.
Wakati  baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, gazeti  la globalpublishers  hili limefanya utafiti wa watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo na lina matokeo ambayo yanaonesha ngoma nzito.

 

Utafiti huo ulioendesha kwa njia ya kura za maoni kwa wasomaji wa gazeti la globalpublishers hili kwa wiki 14 umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli wangekabana koo kwani matokeo yameonesha kutofautiana kidogo kwa kura.



Bw.Lowassa anayewakilisha Jimbo la Monduli ameongoza katika orodha hiyo kwa  kupata kura 759,611 ambazo ni asilimia 34 na Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato amepata kura  692,587 ambazo ni asilimia 31.





Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Bernard Membe amepata kura 235,757 ambazo ni asilimia 11 na amekaribiana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta aliyepata kura 201,074 ambazo ni asilimia 9, kukiwa na tofauti ya asilimia mbili.



Wengine waliopigiwa kura na kura zao katika mabano ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (178,732, asilimia nane), Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi za Afrika, Dk. Salim Ahmed Salim (89,366 asilimia nne) na Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Asharose Migiro (44,683 asilimia mbili).


 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Bernard Membe.


Kura zilizoharibika ni asilimia moja kwani wapo waliokuwa wakichagua zaidi ya jina moja katika sms moja na wengine kuandika majina ya watu ambao hawakuwemo katika orodha ya wapigiwa kura.
 



Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta.


Hata hivyo, baadhi ya wananchi wameshauri kwamba gazeti hili lifanye utafiti mwingine kwa kumpambanisha mgombea huyo wa CCM aliyeshinda na wapinzani.




Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.


Awali wasomaji wetu walichagua wanasiasa mbalimbali kutoka CCM ambao wanafaa kuwa viongozi wa nchi na uongozi wa gazeti hili ukateua wanane waliotajwa mara nyingi na wananchi kisha kuwapambanisha.


Habari Na:globalpublishers


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad