Bw.Deocres
Nsinde(CCM),
Diwani
wa kata ya Buleza,
Wilayani Muleba.
|
Wajumbe wa baraza la madiwani
wa halmashauri ya wilaya hiyo wamebainisha hayo jana wakati wakiwasilisha
taarifa a utekelezaji wa miradi ya mendeleo kwa kipindi cha mwezi januari hadi
februari mwaka huu.
Diwani wa kata ya Buleza Bw. Deocres Nsinde(CCM) alisema kuwa tangu
kata yake iwe katika halmashauri ya wilaya ya muleba haijatengewa bajeti ya
kutengeneza barabara za vijiji katani humo na kusababisha wananchi kukosa
maendeleo ya haraka.
Bw.Nsinde alisema kata hiyo
yenye vijiji vinne vya Butembo ,Buleza,Kihorere na Makarwe vikiwa na jumla ya vitongoji 12 hakuna ofisi
za watendaji wa vijiji na ofisi ya kata hiyo ilitaifishwa na viongozi wa kanisa la Assemblis Of God ambayo
ilikuwa mali ya wakandarasi wa barabara Tanroad mkoani kagera.
Alidai kuwa miundombinu
katika vijiji ni pamoja na uhaba wa vyoo katika shule a msingi na sekondari
madawati vyoo kwa ajili ya wanafunzi hata walimu wao na katika ahanati kwa
ajili ya watafutta huduma a afya , maji pamoja na nyumba a watumishi.
“Mambo haya yanapokosekana
yanaleta udhia na serikali kuwa na wakati mugumu kwa kuttekelea ilani ya ccm ya
maisha bora kwa kila Mtanzania na hili ni kucheleweshwa kwa fedha a ruuku ikiwa
ni pamoja na kutengwa kiasi kidogo katika miradi”.Alisema Nsinde.
Naye diwani wa kata ya Gwanseri
Bw. Julius Rwakyendela (CUF) alisema kuwa shughuli za maendeleo hufanywa na wenyeviti
wa vitongoji ambao hawako katika ajira wala kuwa watambuzi wa sheria katika kusimamia
utawala bora.
Bw.Rwakyendele alisema watendaji
waliopo wanatawalaa maeneo makubwa ya vijiji na kushindwa kusimamia majukumu
yao ipasavyo na kujiingia katika vitendo vya unyanyasaji wananchi kwa kfanya
kazi kwa mazoea.
Alitaja changamoto nyingine
kuwa ni wenyeviti wa vitongoji
kukosa mafunzo elekezi ya kusajili wakazi w vitongoji kwa kutumia vitabu vya
serikali za mitaa kwani baadhi yao hupoteza
takwimu na kusajili wananchi kwa
mianya ya rushwa hasa katika maandalizi ya kupata vyeti vya uraia.
Bi.Oliva Vavunge-DED Muleba. |
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri
ya Wilaya ya Muleba Bi.Oliva Vavunge alikiri kuwa halmashauri hiyo kukumbwa na changamoto za
kiutawala bora na uhaba wa watendaji na kwamba mikakati iliyopo ni kutafuta fedha kutoka vyano vya mapato ili kutoa
mafunzo kwa viongozi wa vijiji kutambua mipaka ya majukumu yao.
Alifafanua kuwa kwa sasa
ajira ya watendaji wa vijiji na kata iko kwa mamlaka ya tume ya ajira nchini na
halmashauri iko katika mpango wa kutuma maombi ya kuajiri kulingana na mapato
yya fedha za kuwalipa mishahara kwa kuzingatia kiwngo cha elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
Na:Shaaban Ndyamukama-Muleba.
No comments:
Post a Comment