Waziri
wa Tawala za Mikoa
na
Serikali za Mitaa, (Tamisemi),
Bi
Hawa Ghasi
|
Rais Jakaya
Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa
lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.
Aidha
amewateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa
wawili kuwa wakurugenzi wa majiji.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mabadiliko ya uongozi yamefanyika
katika halmashauri za majiji ya Arusha, Mwanza, Dar-es- Salaam na Mbeya.
Alisema wakurugenzi
walioteuliwa na kuhamishwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora,
Sipora Liana kuwa Mkurugezni wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa mji wa Njombe,
Hassan Hida kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.
Ghasia
alisema wakurugenzi waliohamishwa ni wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Zungiza
kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Wilson Kabwe,
kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam.
Alisema
kutokana na mabadiliko hayo nafasi za wakurugenzi wa halmashauri za Tabora na
Mji wa Njombe zimebaki wazi.
Pia Waziri
Ghasia alisema kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wakurugeznzi wapya wa
mamlaka za serikali za mitaa kujaza nafasi wazi na kuwabadilisha vituo vya kazi
baadhi ya wakurugenzi.
Aliwataja
wakurugenzi hao kuwa ni pamoja na halmashauri za wilaya walizopangiwa kuwa ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji, Alfred Luanda (Tabora), Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Meatu, Isaya Moses (Njombe), Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda
(Singida), Mkuu wa Idara ya Ujenzi mkoani Mwanza , Boniface Nyambere (Kigoma),
Mwanasheria katika Ofisi ya Tamisemi, Suleiman Lukanga ( Mji wa Mpanda).
Aidha alisema wakurugezni wa mamlaka za
serikali walioteuliwa na halmashauri za wilaya wanazokwenda kuwa ni Hamis Yunah
(Busega), Twalib Mbasha ( Monduli), Musa Natty (Kinondoni), Omari Mkombole
(Babati), Danstan Mallya (Sengerema), Abdallah Kidwanka (Geita), Godwin Benne
(Mlele), William Waziri (Ludewa), Gaudence Nyamwihura (Liwale), Grace Mbaruku
(Lindi), Zabibu Shaban (Pangani), Amina Kiwanuka (Nkinga), Abrahaman Mndeme
(Nzega) Sixtus Kaijage (Songea), Rashid Salim (Rufiji), Mwendahasara Maganga
(Kaimu-Ilala), Paulo Ntinika (Kaimu-Mufindi), Abdallah Malela (kaimu-Bariadi).
No comments:
Post a Comment