Hili ndilo basi la Taqwa baada ya kupata ajali mbaya likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda nchini Zimbabwe, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 06, 2013

Hili ndilo basi la Taqwa baada ya kupata ajali mbaya likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda nchini Zimbabwe, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.


Hili ndilo basi la Taqwa baada ya kupata ajali mbaya ambapo Ajali hiyo iliyahusisha magari matatu ambayo ni basi la Taqwa aina ya Nissan Disel lenye namba za usajili T 273 CBR (Sniper), lori la mizigo aina ya Scania, mali ya Kampuni ya Nyati Transport Ltd lililokuwa limebeba shehena ya viazi pamoja na lori la mizigo lenye namba T 104 BZZ aina ya Scania, mali ya kampuni ya Sogea Satom.




Aidha watu  saba walikufa papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa vibaya baada ya basi hilo la Kampuni ya Taqwa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam –Tanzania kwenda nchini Zimbabwe, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo (May 4, 2013) jioni katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad