UFARANSA:
David Beckham ameweka rekodi ya kutwaa mataji ya Ligi Kuu na klabu za nchi nne
tofauti, baada ya PSG kuifunga Lyon 1-0 na kutwaa ubingwa wa Ligue 1, Ufaransa.
Beckham,
ambaye sasa anakuwa mchezaji wa kwanza wa Uingereza kutwaa mataji katika nchi
nne tofauti, aliingia akitokea benchi, wakati Jeremy Menez alipokifungia bao
pekee la ushindi kikosi cha Carlo Ancelotti.
Ubingwa
wa PSG hautathibitishwa hadi Kamati ya Nidhamu ya Ligi itakapokutana kuamua
kuipokonya pointi au la kufuatia tuhuma za Mkurugenzi wake, Leonardo kumrubuni
refa.
|
No comments:
Post a Comment