![]() |
Judith
Wambura 'Lady Jaydee'.
|
Mwanamuziki Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady
Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo.
Katika hati
ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group
ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.
Tuhuma za
kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei
27 mwaka huu.
Jaydee
aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6
mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao
aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.
No comments:
Post a Comment