![]() |
Bunduki moja
aina ya SMG na risasi 16 iliyokamatwa na jeshi la Polisi Mkoani Kagera.
|
![]() |
Kaimu
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe akionyesha bunduki na risasi
zilizokamatwa.
|
Polisi
mkoani Kagera wamewakamata watu wanane wanaosadikiwa kuwa ni majambazi sugu,
ambao wamekuwa wakitafutwa kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali ya
uhalifu ikiwemo utekaji wa magari maeneo ya porini na uporaji wa mali za
wafanyabiashara.
Kaimu
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe anasema kwa muda mrefu polisi
wamekuwa wakifuatilia mtandao wa majambazi wanaojificha katika mapori, ambapo
huteka magari na kupora mali za wafanyabiashara.
Anawataja
waliokamatwa kuwa ni pamoja na mwanamke mmoja Leoncia Rovast (28), ambaye
anadaiwa kuwa kinara wa kupanga mipango ya utekaji na uporaji.
Watuhumiwa
wengine kuwa ni Iman Ezekiel (24), Ndanda Iliofu (24), Hanana Francis A.KA
Baseka (26) Kabichi Sylivestar (23), Slambuki Abel (25) na Amos Amos (30) A.K.A
Rasi.
Wengine ni
Sabuhalo Daud (26) ambaye anatuhumiwa kuhusika na utunzaji wa mali na vifaa
vinavyoporwa baada ya utekaji, ambapo alikutwa na bunduki moja aina ya SMG na
risasi 16.
No comments:
Post a Comment