![]() |
Rio Ferdinand. |
Beki
wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand
ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa kwa madai kwamba anataka
kujihusisha zaidi na klabu yake.
Ferdinand
mwenye umri wa miaka 34, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Uingereza mechi 81
amesema kabla ya kutoa uamuzi huo alikiria kwa kipindi kirefu na kuona wakati
wa yeye kustaafu soka la kimataifa umefika.
Ferdinand
hajacheza mechi yoyote ya Uingereza toka katika mchezo wa kufuzu michuano ya
Ulaya 2012 dhidi ya Switzerland Juni 2011 ambapo Roy Hodgson alimuita katika
mechi ya kufuzu dhidi ya Kombe la Dunia dhidi ya San Marino na Montenegro Machi
mwaka huu lakini alijitoa kwasababu ya kusumbuliwa na maumivu ya mgongo.
Nyota
huyo ambaye ameisaidia klabu yake kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu huu amesema
wakati wa kupisha damu changa katika timu ya taifa umefika ili naye aweze
kupata nafasi ya kuongeza nguvu zake kuitumikia klabu yake.
RIO
FERDINAND AKIWA NA TIMU YAKE YA UINGEREZA.
-1997:
Aanza kuichezea England Mechi na Cameroon Uwanjani Wembley
-1998:
Ateuliwa Kikosi cha England Kombe la Dunia lakini hakucheza
-2000:
Atemwa Kikosi cha Euro 2000
-2002:
Aifungia England Bao walipoifunga Denmark 3-0 katika Kombe la Dunia
-2004:
Afungiwa Miezi 8 kwa kukosa kupimwa Madawa yanayokatazwa
-2006:
Acheza Mechi 5 katika Kombe la Dunia huko Germany
-2008:
Awa Nahodha wa England kwa mara ya kwanza
-2010:
Terry avuliwa Unahodha na kukabidhiwa Ferdinand lakini ashindwa kucheza Fainali
za Kombe la Dunia baada ya kuumia
-2011:
Acheza Mechi yake ya 81 dhidi ya Uswisi kwenye Mchujo wa EURO 2012
-2012:
Atemwa EURO 2012
-Machi
2013: Anaitwa tena kuichezea England Mechi za Kombe la Dunia lakini anajitoa
kutokana na kukabiliana na majeruhi yake ya muda mrefu
-Mei
2013: Atangaza kustaafu kuichezea England
Akiongelea
kustaafu kwa Rio, Meneja wa England Roy Hodgson alisema: "Kwa kuwa Nahodha
wa Nchi yake, kucheza Fainali za Kombe la Dunia 3, kunamfanya awemo katika
kundi la Wachezaji spesho!."
Mara
ya mwisho kwa Rio Ferdinand kuichezea England ilikuwa Juni 2011 walipocheza na
Uswisi kwenye Mechi ya Mchujo ya EURO 2012.
Msimu
huu, Ferdinand aliibuka upya baada ya kupona maumivu ya mara kwa mara aliyokuwa
akipata huko nyuma, na kuiongoza Klabu yake Manchester United kutwaa tena Taji
lao la Ubingwa wa Uingereza.
Akiongea,
Rio Ferdinand alisema: “Nadhani huu ni wakati muafaka kung’atuka na kuwaachia
Vijana na mimi nibakie kuichezea Klabu yangu tu.”
Kesho
Alhamisi(May 16,2013), Roy Hodgson anatarajiwa kutangaza Kikosi cha England kitakachocheza
Mechi za Kirafiki za Kimataifa na Republic of Ireland Uwanjani Wembley hapo Mei
29 na hapo Juni 2 kucheza huko Nchini Brazil Mjini Rio De Janeiro kwa
kukabiliana na Brazil.
No comments:
Post a Comment