Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe akiangalia moja ya nyumba siyobora wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo wilayani Biharamulo ,mkoani Kagera(Picha na Shabani Ndyamukama). |
Mfano wa Nyumba bora ambazo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe amewataka Viongozi wa Kiserikali na Vyama vya Siasa mkoani humo,kuwahamasisha wananchi Kujenga nyumba za mfano huo. |
Mfano wa Nyumba bora ambazo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe amewataka Viongozi wa Kiserikali na Vyama vya Siasa mkoani humo,kuwahamasisha wananchi Kujenga nyumba za mfano huo. |
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe amewataka Viongozi wa Wilaya Mkoani
Humo ,ndani ya miezi sita
kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo hasa ardhi
na misitu kujenga nyumba bora za kuishi kuliko zile za matembe kuonekana kuwa
maskini bila kufanya kazi na kujiletea maendeleo.
“Makazi hayo
yajengwe kwa kutumia matofali yasiyochomwa na kuezekwa kwa miti na nyasi kisha
waongeze uzalishaji wa mazao ya kilimo na ufugaji ndani ya mwaka mmoja waezeke
kwa mabati” Alisema Masawe.
Akiwa katika ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika wilaya za Biharamulo na Ngara mkoani humo, Kanali Masawe
alishauri ukusanyaji wa michango ya
wananchi katika kujiletea maendeleo mkoani Kagera , uzingatie kutolewa
rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao kuliko madai ya fedha ambazo
huliwa na watendaji wasio waaminifu katika Vijiji na Kata kwa kukosa kuwapatia
stakabadi halali wala taarifa ya mapato na matumizi.
Aliwataka Maafisa
ugani kuhakikisha wanafanya kazi zao Vijijini kuwasaidia utaalamu Wakulima na Wafugaji
ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri kuwachukulia
hatua Walevi saa za kazi pamoja na Wasiowajibika ipasavyo.
No comments:
Post a Comment