Jose Mourinho. |
Meneja wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Jose
Mourinho amekiri kuwa FC Barcelona wamestahili kunyakuwa taji la Ligi Kuu ya
nchi hiyo maarufu kama La Liga, kufuatia sare ya bao 1-1 iliyopata timu yake
dhidi ya Espanyol jana(May 11,2013).
Espanyol,
wakicheza Nyumbani, walitangulia kufunga Bao kupitia Christian Stuani katika
Dakika ya 23 na Gonzalo Higuain kuisawazishia Real kwenye Dakika ya 58.
Katika
mchezo huo Real Madrid walishindwa kutamba ugenini baada ya kujikuta
wakitangulia kufungwa na wenyeji wao kabla ya mchezaji Gonzalo Higuain kusawazisha lakini walishindwa
kuongeza bao lingine ili kuhakikisha wanabakia katika mbio za Ubingwa.
Kocha Mourinho
mwenye umri wa miaka 50 amesema anaipongeza Barcelona, makocha wao, wachezaji
na mashabiki kwa kazi kubwa na yenye mafanikio waliyofanya katika msimu huu
mpaka kuhakikisha wanatawadhwa mabingwa wapya wan chi hiyo.
Mbali na kuipongeza Barcelona,Kocha Mourinho pia alionyesha kukasirishwa na swali aliloulizwa na mwandishi kuhusu sakata la kumuacha katika kikosi cha kwanza nahodha Iker Casillas akidai kuwa akiwa kama kocha hapaswi kutoa sababu yoyote kuhusiana na hilo.
Mourinho
amesema kwasasa ligi ina Bingwa mpya hivyo anashangaa watu wanapozungumzia
mchezaji mmoja, kwani yeye akiwa kama kocha ana uhuru wa kuchagua nani acheze
na nani asicheze hivyo haoni kama swali hilo lilikuwa na maana.
Hata hivyo,
Mourinho huenda akalazimika kumchezesha Pepe Ijumaa ijayo kwenye Fainali ya
Copa del Rey kwa vile Mtu aliemyang’anya namba, Raphael Varane, huenda asiwe
fiti baada ya kuumia.
Alipoulizwa
hilo, Mourinho alijibu: “Ijumaa mtaona nani atacheza na huo utakuwa uamuzi
wangu.’
Leo(May
12,2013) , Mabingwa wapya wa La Liga, FC Barcelona, watasafiri kwenda Madrid kucheza na
Atletico Madrid kwenye Mechi ya La Liga.
No comments:
Post a Comment