Roberto
Martinez's men have won the FA Cup for the first time in their history after
stunning Manchester City at Wembley courtesy of a last minute header from the
midfielder.
|
Mchezaji Pablo Zabaleta alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi za njano mbili katika dakika ya 84 ya mchezo huo. |
Kocha
Roberto Mancini akiwa na Manchester City kucheza Fainali ya FA CUP dhidi ya Wigan Athletic katika uwanjani Wembley ameshindwa kutwaa Kombe lake la 3 katika
Misimu mitatu akiwa na Man City baada ya kukubali kufungwa bao 1 – 0 na Wigan Athletic katika Fainali ya FA CUP leo
(May 11,2013.
Kukosa
kombe hilo huenda likamuweka Kocha Roberto Mancini , katika wakati mgumu ndani
ya Man City ,kwani Wachambuzi wamedai huenda akatimuliwa Man City mara baada ya
kuupoteza Ubingwa wao wa Ligi kuu Soka Uingereza uliochukuliwa na Manchester
United Msimu huu 2012/2013.
Kwa
mujibu wa ripoti kutoka huko nchini Hispania ,Kocha Manuel Pellegrini atakuwa
Meneja mpya wa Manchester City Msimu ujao kwa kumbadili Robertu Mancini.
Ripoti
hizo zinadai Man City italipa Pauni Milioni 3.4, ikiwa ni kutimiza Kipengele
cha kuvunja Mkataba, ili kumchukua Pellegrini kutoka Klabu yake ya Malaga
inayocheza La Liga.
Mchezaji
Pablo Zabaleta alitolewa kwa kadi
nyekundu baada ya kupata kadi za njano
mbili katika dakika ya 84 ya mchezo huo.
Wigan
ambayo ipo hati hati kushushwa Daraja katika Ligi
kuu, wanabeba FA Cup ikiwa ni Historia
kwao kwani Hii ni Fainali ya 10 kwa Man
City kwenye FA CUP na wametwaa Kombe hili mara 5 katika Miaka ya
1904, 1934, 1956, 1969 na 2011 huku kwa Wigan ni Fainali ya kwanza tangu Timu yao
ianzishwe Mwaka 1932.
Kwa
Kuwa Mshindi , Wigan Athletic sasa
atacheza Mashindano ya Europa League msimu ujao wa 2013/2014 huku Man City
wameshafuzu UEFA Champions League msimu ujao kwa kutwaa nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa
Manchester United kwenye Barclays Premier League.
No comments:
Post a Comment