Suleiman Kova |
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Suleiman
Kova amesema Taarifa zilizoenea kwamba
Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT),
Kunduchi jijini Dar es Salaam leo(May 11,2013) zimeenea ndivyo sivyo na kwamba
askari walikuwa wanapambana na majambazi.
Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya
kijamii na mitaani kwamba kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi
punde, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema
kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa
wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment