![]() |
Borrusia
Dortmund wakiwasili Jijini London mapema leo(May 24,2013).
|
![]() |
Roberto
Lewandoski na wenzie ndani ya Heathrow Airport Jijini London mapema leo(May
24,2013).
|
![]() |
Mario Gomez
akiwasili Jijini London mapema leo(May 24,2013) in the Champions League final kati ya Bayern Munich dhidi ya Borussia Dortmund hapo kesho (May 25,2013).
|
![]() |
Jurgen Klopp
kocha wa Borrusia Dortmund ndani ya Heathrow Airport Jijini London mapema leo(May
24,2013) in the
Champions League final..
|
![]() |
Frank Ribery
akilakiwa na umati wa mashabiki Jijini London mapema leo(May 24,2013) in the final kati ya Bayern Munich dhidi ya Borussia Dortmund hapo kesho (May 25,2013).
|
Ijumaa(May
24,2013) UEFA imetangaza kuwa Bingwa wa
Mashindano ya Europa League atazawadiwa
kwa kuingizwa moja kwa moja kucheza Mashindano makubwa ya Champions League kuanzia
Mwaka 2016 ili kuboresha Europa League na kuifanya ionekane
muhimu.
Hatua
hii inalenga kuifanya michuano ya Europa League ionekane ni muhimu badala ya
kupondwa na kuonekana ni ngazi ya chini ya Champions League.
Uamuzi
huu umefikiwa baada ya Majadiliano ya muda mrefu kati ya European Club
Association (ECA), Chama cha Klabu Ulaya na UEFA.
Mabingwa
wa Europa League.
-2013:
Chelsea
-2012:
Atletico Madrid
-2011:
FC Porto
-2010:
Atletico Madrid
-2009:
Shakhtar Donetsk
-
Europa
League huingiza Mapato kidogo na huwa na msisimko mdogo ukilinganisha na
Champions League.
-Timu
zinazomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya Champions League hutupwa kucheza Europa League.
-Katika
Fainali ya Mwaka huu ya Europa League iliyokutanisha
Timu zilizobwagwa kutoka Champions League, Chelsea iliifunga Benfica Bao 2-1
huko Amsterdam ArenA, Uholanzi Wiki iliyopita.
Wakati
huo huo, UEFA imetangaza kuwa Mwaka 2015 Uwanja wa Olimpiki wa Berlin huko
Germany ndio utachezwa Fainali ya Champions League na ule wa Mjini Warsaw huko
Poland, wa National Stadium, ndio utachezwa Fainali ya Europa League.
![]() |
Bayern Munich coach Jupp Heynckes |
Mipango
mingine ambayo inajadiliwa na UEFA ambayo itakuwa na Mkutano wa Kongresi yake
hapo Ijumaa Mjini London ikiwa ni Siku moja tu kabla Fainali ya Champions
League kuchezwa Uwanja wa Wembley Jijini humo kati ya Borussia Dortmund na
Bayern Munich, ni pamoja na kuziongezea Ligi kubwa za Ulaya nafasi za
uwakilishi kwenye Champions League kuwa 5 badala ya 4 na kuongeza nafasi za
kucheza Europa League.
Pia,
UEFA inataka kuondoa ule mtindo wa Timu zikiwa Mabingwa wa Champions League na Europa League lakini hazikumaliza Ligi zao zikiwa
zimefuzu kucheza Ulaya wao kucheza Ulaya badala ya zile Timu zilizomaliza Ligi
Nafasi za juu na badala yake kuzibakisha Timu za juu kwenye Ligi kucheza Ulaya
na Mabingwa Watetezi kuingia kutetea Mataji yao.
Uamuzi
huu utaondoa hali iliyowakuta Tottenham Msimu wa Mwaka 2011/12 kwani walimaliza
BPL, Barclays Premier League, wakiwa Nafasi ya 4 na Chelsea kumaliza Nafasi ya
6 lakini Nafasi yao kucheza Champions League ikachukuliwa na Chelsea kwa vile
walitwaa Ubingwa wa Champions League na Tottenham kutupwa Europa League.
Sheria
zote hizi mpya zinatarajiwa kupitishwa Ijumaa huko London UEFA Kongresi
itakapoketi na kuanza kutumika Mwaka 2016.
Pia
UEFA imepitisha Adhabu kwa Kosa la Ubaguzi kuwa Kifungo cha Mechi 10 au zaidi,
kumtukana Mwamuzi kutoka Mechi 2 hadi 3 au zaidi na kumshambulia Mwamuzi si
chini ya Mechi 15 badala ya 10.
Sheria
hizi mpya za Adhabu zitaanza Juni 1.
No comments:
Post a Comment