![]() |
Mwili
wa marehemu ,
Albert Kenneth Mangwea |
Kifo cha
msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea au Mangwair
kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’,
kimeendelea kuwagawa Watanzania katika makundi na kusababisha utata, Ijumaa
linakuhabarisha.
Kwa mujibu
wa ripoti za awali za tukio hilo, Ngwea na mwenzake M 2 the P walizimika wakiwa
usingizi ambapo wote walikimbizwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
katika Hospitali ya St. Helen Joseph nchini humo.
Ilidaiwa
kuwa katika harakati hizo ilithibitika kwamba Ngwea alishafariki dunia huku
mwenzake akiwa hoi bin taaban.
Hata hivyo,
hospitali hiyo haikueleza chanzo cha kifo hicho kwa sababu ya kusubiri uchunguzi
wa mwili wa marehemu.
Habari za
kifo cha msanii huyo zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii huku kila
mtu akisema lake juu ya tukio hilo baya kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo.
Ilisemekana
kuwa kabla ya kukutwa na mauti, staa huyo wa ngoma ya Mkasi alikuwa nchini humo
kwa ziara za kimuziki ambapo Jumanne iliyopita ndiyo ilikuwa arejee Bongo.
MADAI MAZITO
KUTOKA SAUZI.
Katika tukio
hilo lililowagawa Watanzania, baadhi ya watu walidai kuwa inawezekana staa huyo
aliuawa ili adhulumiwe mzigo wa ‘unga’ na watu waliokuwa wamempa tenda ya
kuufikisha nchini humo huku wengine wakisema walijiovadozi na pombe kali.
“Katika hali
ya kawaida inawezekanaje watu wawili wakajiovadozi kwa wakati mmoja? Kama ni
ulevi, huo ni ulevi wa aina gani? Haiwezekani watu walewe sawa kisha wazimike
sawa.
“Hapa kuna
dalili ya kuwepo kwa mchezo mchafu. Kifo
cha Ngwea kina harufu ya kudhulumiana kwenye mzigo, si unajua siku hizi ndizo
dili za baadhi ya wasanii wetu?” alidai Baba P kwenye mtandao wa Twitter.
ALIJIDUNGA
MADAWA YA KULEVYA?
Madai
mengine mazito ni kwamba eti wawili hao walijidunga madawa ya kulevya ambayo
inasemekana yalikuwa feki au famba kama wanavyosema watu wanaodili na unga.
Kuhusu hilo
ilidaiwa kuwa huenda unga waliokutana nao siku hiyo ulikuwa ‘kitu orijino’
tofauti na ule wa Kinondoni, Dar hivyo dozi iliwazidi.
Iliendelea
kusemekana kuwa ukijiovadozi ‘kitu cha Sauzi’ huwa mtumiaji anagonga ‘kick’
kama wanavyosema watumiaji ambapo kitaalam huweza kusababisha kusimama ghafla
kwa mapigo ya moyo kisha kifo.
KUZIDISHA
BANGI?
Wapo
waliodai kuwa huenda jamaa hao walizidisha matumizi ya kilevi cha bangi ambapo
mjadala ulikuwa mkubwa, wengi wakihoji kama kuna uwezekano wa kilevi hicho
kusababisha kifo.
“Nijuavyo
mimi mtu akivuta bangi sana huweza kupata madhara katika ubongo lakini siamini
kama inaweza kuua,” alisema Juma Kisaki akichangia juu ya kifo hicho mtandaoni.
ALILALA,
ASUBUHI HAKUAMKA.
Kwa mujibu
wa watu waliokuwa na Ngwea katika nyumba aliyofikia kwa rafiki yake, jamaa huyo
alilala vizuri lakini cha ajabu asubuhi hakuamka kama walivyopanga kwani
alikuwa asafiri siku hiyo kurudi Bongo.
“Inawezekanaje
mtu alale bila tatizo halafu afe usingizini? Kwa vyovyote kuna kitu. Au labda
walipuliziwa sumu chumbani? Kwani hakukuwa na watu wengine ambao waliamka
salama? Kweli ni utata juu ya utata,” aliandika Anonymous kwenye mtandao wa
Twitter.
KWA NINI
UTATA?
Ni utata kwa
sababu hakuna uhakika wa moja kwa moja kwamba nini kilichukua uhai wa msanii
huyo maarufu Bongo matokeo yake kila mtu anasema lake.
MAMA MANGWEA
ANASEMAJE?
Akizungumza
na ripota wa Ijumaa mjini Morogoro, Dustan Shekidele, mama mzazi wa Ngwea,
Denisia Mangwea (63), alisema kitendo cha mwanaye huyo kumuahidi kwenda
Morogoro kulifanyia ukarabati kaburi la marehemu baba yake kitabaki kichwani
mwake kwa muda mrefu.
Akiwa
nyumbani kwake Kihonda, Mazimbu Road, mama huyo alisema siku za karibuni
aliongea na mwanaye kwa njia ya simu na kumuahidi kwenda Moro kulifanyia
ukarabati kaburi la baba yake, marehemu Kenneth Mangwea.
”Albert
aliniambia angekuja Morogoro wiki ijayo baada ya kutoka Afrika Kusini, leo
(Jumatano) naambiwa naletewa maiti ambayo tutaizika jirani na kaburi la baba
yake?” alihoji na kuangua kilio.
Mama huyo
alisema kuwa Ngwea ni mwanaye wa sita na wa mwisho aliyemzaa mwaka 1982 ambaye
hajawahi kumwambia kama ana mchumba au mtoto.
HALI YA
MWILI WA MAREHEMU.
Ijumaa
lilifanikiwa kupata picha ya mwili wa marehemu. Kwa kuutazama tu alitokwa na
damu puani na masikioni wakati akikata roho.
POMBE KALI
ZAKUTWA CHUMBANI.
Ilidaiwa
kuwa ndani ya chumba alicholala Ngwea kulikuta bapa (chupa) mbili za pombe kali
aina ya Vodka hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini pombe zilichangia
kusindikiza kifo hicho.
RIPOTI FEKI
YASAMBAA MTANDAONI.
Katika hali
ya kushangaza, juzi baadhi ya mitandao iliweka ripoti inayodaiwa ni feki.
Katika
ripoti hiyo, ‘madaktari’ waliouchunguza mwili wa Ngwea walibaini kwamba kabla
ya kifo chake yeye na mwenzake walizidisha kileo na unga.
Pia wawili
hao eti hawakuwa na mpangilio mzuri wa chakula kwa maana kwamba walikuwa
wakinywa pombe kali bila kupata msosi wa nguvu kama ‘nyama choma’.
![]() |
Msanii
Albert Mangwea akifanya makamuzi ndani ya Dar Live enzi za uhai wake.
|
![]() |
Ngwair
(kulia) katika pozi na wasanii wenzake Ommy Dimpoz na Diamond.
|
![]() |
Ngwair
akipozi na TID.
|
KAULI YAKE
YA MWISHO.
Mangwea,
siku moja kabla ya kifo chake aliandika kwenye ukurasa wake katika Mtandao wa
Kijamii wa Twitter hivi: “Love Him who died for us, Yeshus a.k.a Jesus, King of
all Kings, Amen.”
Tafsiri
rahisi ya maneno hayo ni: “Mpende Yesu ambaye alikufa kwa ajili yetu, mfalme wa
wafalme, Amen.”
Baadaye tena
akaandika: “Mambo matano muhimu ya kumfanya demu wako akupende; 1 – mpe hela, 2
– mpe hela, 3 – mpe hela, 4 – nakwambia we mpe hela, 5 – we mpe hela tu
utaona.”
Chanzo:GPL.
No comments:
Post a Comment