![]() |
Neymar. |
FC Barcelona wamefanikiwa kushinda mbio za kumsaini nyota wa Brazil Neymar kwa ada ya
uhamisho ya £20 million kwa mkataba wa
miaka mitano.
Mshambuliaji
huyo sasa anaelekea barani ulaya baada ya Santos kukubali kumuuza nyota wao
waliomng'ang'ania kwa miaka mingi.
Akiandika
kwenyepage yake ya Instagram, Neymar alisema: "Nimeongea na marafiki na
familia. Jumatatu nitajiunga na Barcelona."
Mabosi wa
Barca walienda Sao Paolo kwa mazungumzo mazito kuhusu usajili wa mbrazili huyo,
na wakafanikiwa kuwashawishi Santos kumuuza Neymar ambaye angeweza kuondoka
bure mwezi Julai.
Neymar
alitaka muda kufikiria ofa nyingine kutoka kwa wapinzani wa Barcelona, Real Madrid
lakini mwishoni akaamua kwenda Nou Camp.
Kwa usajili
huu sasa Neymar atajiunga na star wa Argentina Lionel Messi na kuunda
safu ya ushambuliaji inayotisha barani ulaya.
Neymar
ameifungia Santos mabao 138 kwenye mechi 229 tangu mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment