Utafiti huo
wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe
walioipenda ijulikanayo kama Luwombo kwa
asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.
Kwa mujibu
wa utafiti huo,Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52,ikiwa
nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07. Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa
kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia
3.77, kwa wa watu wake kunywa za asili.
Ripoti ya
utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia
pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.
Mtaalamu wa
masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa , eti
aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo zenye historia ndefu kwa
sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama kwa wazungu.
Alisema hali
hiyo inahatarisha usalama wa afya za wageni watakaoonja pombe hizo.“Watanzania
waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia
sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini,moyo
,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza, lakini hakusema kuwa
jambo hili pia linatokea kwa pombe za
kizungu.
Dk pia alipinga juu matumizi ya pombe katika
kuondoa msongo wa mawazo.“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo,
inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” Japo wote
tunajua kuwa kusahau ni aina ya kupunguza mawazo.
Aliongeza
kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo
cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya
afya. Kwa mfano kama huna ada ya shule kwa wanao nenda kituo cha afya upate
ushauri nasaha, utaondoa msongo.
Katika miaka
ya hivi karibuni,kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji
pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine.
Hapa tunazungumzia pombe za kiafrika tu za kizungu kunyweni ni safi zana kwa
kuondoa msongo wa mawazo.







No comments:
Post a Comment