Kuna nafasi
tunaweza tukashuhudia El Classico kwenye fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya
kwenye dimba la Wembley baada ya Real Madrid na Barcelona kutengenishwa kwenye
droo ya nusu fainali iliyofanyika muda mchache uliopita jijini Geneva Uswis.
Kikosi cha
Jose Mourinho Real Madrid kimepangwa kucheza dhidi ya Borussia Dortmund wakati
Barcelona wamepangwa kucheza na Bayern Munich, hivyo kumaanisha kwamba ikiwa
wapinzani wa ligi mbili tofauti - Spain na Ujerumani wanaweza kukutana kwenye
fainali ya Wembley May 25.
Dortmund
ndio timu pekee ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye michuano hii, na
watacheza na Real kwa mara pili ndani ya msimu huu wa UCL. Dortmund waliweza
kushinda na kuongoza kundi gumu lilokuwa likihusisha timu za Real, Manchester
City na Ajax.
Mabingwa wa
sasa wanaosubiri kuvikwa taji tu la Bundesliga
Bayern Munich wapo kwenye form ya kutisha msimu huu, wakitoka kuikanyaga
Juventus nyumbani na ugenini.
Mechi za
kwanza za nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya zitachezwa April 23 na
April 24, na marudiano zitafanyika wiki inayofuatia tarehe April 30 na May 1.
Wakati kwa
upande wa UEROPA LEAGUE - Chelsea wamepangwa na FC Basel wakati Fenerbahce watakipiga na Benfica.
Mechi hizo
za Nusu Fainali zitachezwa kwa mtindo wa Nyumbani na Ugenini na Mechi za kwanza
zitachezwa Alhamisi Aprili 25 na Marudiano Alhamisi Mei 2.
Fainali
itakayochezwa Jumatano Mei 15 ndani ya Amsterdam ArenA kuanzia Saa 3 Dakika 45
Usiku, kwa saa za Africa ya Mashariki.







No comments:
Post a Comment