Wakulima wauza zao la ndizi wilayani Ngara Mkoani Kagera wameaswa kuboresha kilimo cha zao la migomba ili waweze kufanikiwa katika ushindani wa mauzo ya zao hilo . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 12, 2013

Wakulima wauza zao la ndizi wilayani Ngara Mkoani Kagera wameaswa kuboresha kilimo cha zao la migomba ili waweze kufanikiwa katika ushindani wa mauzo ya zao hilo .

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo  ya siku 3 kwa  Vikundi vya Wakulima wauza Ndizi  yanayofanyika katika Ukumbu wa Idara ya Kilimo Wilayani Ngara mkoani Kagera.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo  ya siku 3 kwa  Vikundi vya Wakulima wauza Ndizi  yanayofanyika katika Ukumbu wa Idara ya Kilimo Wilayani Ngara mkoani Kagera.
Aliyesimama ni Afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Bi. Adelina Mapunda


Wakulima wauza wa zao la ndizi wilayani Ngara  Mkoani kagera wameaswa kuboresha  kilimo cha zao la migomba  ili waweze kufanikiwa katika ushindani wa mauzo ya zao hilo .





Afisa ushirika wa

 halmashauri ya wilaya

 ya Ngara

Bi. Adelina Mapunda

na

Bw. Edisoni Mhagama

 katika Mafunzo hayo ya

 Siku 3 katika ukumbi wa

 idara ya Kilimo mjini Ngara.
Afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Bi. Adelina Mapunda amesema kuwa wilaya hiyo imezungukwa na wazalishaji wa mazao ya ndizi ikiwemo nchi za Burundi na Rwanda hivyo Wazalishaji hao  hawana budi kuboresha huduma zao ikiwemo ubunifu wa kutengeneza bidhaa zinazo tokana na zao la ndizi. 




Aidha amewataka Wakulima  hao kuungana pamoja na kudumisha ushirikiano  ili umoja wao uwezi kuimarika katika shughuli za mauzo ya mazao yao ikiwemo kusafiri nje ya mkoa wa kagera ili kujifunza ushindani  uliopo katika uuzaji wa zao la ndizi.




Katika hatua nyingine Bw. Edisoni Mhagama ambaye ni Muwezeshaji katika Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na  SIDO pamoja na Shirika la BTC,   amewataka kuunda Vikundi vya Ujasirimali ili kupata mikopo itakayowawezesha kukabili changamoto mbalimbali  za kilimo cha zao la Ndizi .




Mafunzo hayo ya siku 3 kwa  Vikundi vya Wakulima wauza Ndizi  yanafanyika katika Ukumbu wa Idara ya Kilimo Wilayani Ngara mkoani Kagera.


Bw. Edisoni Mhagama ambaye ni Muwezeshaji katika Mafunzo hayo Chini ya  SIDO , yaliyodhaminiwa na Shirika la BTC.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo  ya siku 3 kwa  Vikundi vya Wakulima wauza Ndizi  yanayofanyika katika Ukumbu wa Idara ya Kilimo Wilayani Ngara mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad