![]() |
| Suarez |
Mshambuliaji
huyo wa Liverpool ambaye haiishi vituko uwanjani jana alikiri kwamba alifanya
kweli shambulio hilo.
Aidha leo hii(April 24,2013) FA wamemaliza msimu wake kwa kumpa adhabu ya
mechi 10.
Kwa kawaida adhabu ya kitendo cha vurugu huwa ni mechi zisizodi 3 lakini wamesema kwamba adhabu hiyo haitoshi kwa Suarez ambaye amekuwa mtukutu kwa matukio ya ajabu ajabu kila mara.
Suarez jana usiku alikataa kukubaliana na adhabu ya zaidi ya mechi 3. Lakini leo FA wameamua vinginevyo kwa bad boy Suarez na hivyo atakumbana na adhabu ya kutocheza mechi 10 za mashindano yaliyo chini ya FA.
![]() |
|
Chama cha soka cha England kimetangaza kufungiwa kwa mchezaji
Luis Suarez kwa mechi 10 kwa kosa la kumng'ata Branslav Ivanovic katika mchezo
wa ligi kuu ya England wiki iliyopita.
|
Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alisema: "Sote klabu na mchezaji husika tumeshtushwa na kutopendezewa na maamuzi haya - tunasubiri sababu za kimaandishi kabla hatujatoa uamuzi wowote hapo kesho."
Suarez ana muda mpaka Ijumaa kupinga adhabu hiyo kwa kukata rufaa.
Huko nyuma
kumekuwepo na matukio ya vurugu uwanjani yaliyofanywa na wachezaji na adhabu
zake zikaishia katika kufungiwa mechi kadhaa - sasa tujaribu kuangalia matukio
hayo na adhabu zilizotolewa na kufananisha na hii ya sasa Suarez.
ADHABU YA
MECHI 12.
Duncan
Ferguson (Rangers):
Mchezaji huyu alipewa adhabu ya kufungiwa mechi 12 kwa kumpiga kichwa mchezaji
wa Raith aitwaye John McStay mnamo mwaka 1994.
Joey Barton (QPR): Mtukutu Joey Barton nae yupo katika nafasi ya kwanza kwa kufungiwa mechi 12 kwa kumpiga kichwa mchezaji wa Manchester City katika mechi ya mwisho ya ligi kuu msimu uliopita.
MECHI 11.
Paolo Di
Canio (Sheffield
Wednesday): Kocha wa sasa wa Sunderland ni mmoja kati ya wachezaji watukutu
ambao wameshawahi kucheza kwenye ligi kuu ya England - mnamo mwaka 1998 alimsukuma
refa Paul Alcock na kwa kitendo hicho akafungiwa mechi 11.
MECHI
10 .
Kevin
Keegan (Liverpool)
na Billy Bremner (Leeds): hawa magwiji wa soka walifungiwa mechi 10 kwa
kitendo chao cha kupigana katika mechi ya kombe la hisani mwaka 1974.
David Putton (Southampton): Kama ilivyokuwa kwa Di Canio - Alan Wiley nae alimsukuma refa mwaka 2005 na akafungiwa mechi 10.
MECHI 9.
Paul
Davis (Arsenal):
Alifanya kosa la kumpiga ngumi Glenn Cockerill mwaka 1998.
Steve Walsh (Leicester) kwa utovu wa nidhamu mnamo mwaka 1987.
MECHI 8.
Luis
Suarez (Liverpool):
Kwa kumtolea matusi ya kibaguzi mchezaji wa Manchester United Patrice Evra
mnamo mwaka 2011.
Ben Thatcher (Manchester City): Kwa kosa la kumpiga kiwiko Pedro Mendes mwaka 2006.
Mark Dennis (QPR): Alifungiwa mwaka 1987 kwa kupata kadi nyekundu ya 11 ndani ya ligi kuu ya England.
Habari
Na:Mwana wa Makonda
Na
shaffihdauda.









No comments:
Post a Comment