Hongera Man United! Ushindi wa kishindo na mmestahili kuwa Mabingwa wa Ligi kuu soka Uingereza . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 23, 2013

Hongera Man United! Ushindi wa kishindo na mmestahili kuwa Mabingwa wa Ligi kuu soka Uingereza .



RvP claps the incredible

crowd at Old Trafford.
Manchester United imetwaa rasmi ubingwa wa 20 wa taji la ligi kuu soka nchini Uingereza  kwa ushindi wa mabao matatu ya aina yake dhidi ya Aston Villa,Mabao yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie ambaye sasa atakuwa akiongoza safu ya wafungaji kwa kufikisha mabao 24 huku Luis Suarez akifuatia akiwa na mabao 23.



Robin van Persie  ambaye alikuwa ni Nahodha  wa Arsenal na bila kutwaa Ubingwa wowote na Arsenal , aliamua kuhamia Manchester United Msimu huu  ili awe Bingwa, akapewa Namba 20 kwenye Jezi yake , alipiga Bao 3, ambazo ni Hetitriki  na kuipa Man United Ubingwa wa 20 na kuweka Historia mpya Uingereza huku  United wakiwa na Mechi 4 mkononi.





Hii imekuwa mara ya nne kwa Manchester United kutwaa Ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Traford,baada ya kufanya hivyo mwaka 1999,2002 na 2009. 




Mara ya mwisho Manchester  United kutwaa ubingwa wa ligi kuu huku wakiwa na michezo mingi iliyosalia ilikuwa mwaka 2001 baada ya kutangazwa mabingwa huku wakiwa na michezo mitano kibindoni.


Phil Jones celebrates with a Champions flag — at Old Trafford - Manchester United.


Title celebrations on the pitch
Old Traford.



Giggs and Ferdinand celebrating on the pitch last night like it was their first title! In fact Giggsy has featured in all 13 United title-wins...Legend!




Jonny Evans na Sir Alex
Huu ni ubingwa wa 13 wa taji la ligi kuu ya Uingereza kwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo mwaka 1986.





Kwa matokeo hayo ya Aston Villa kufungwa mabao 3-0  Uwanjani Old Trafford watasalia kwenye nafasi ya 17 wakiwa na pointi zaidi ya timu ambazo zipo kwenye hatihati ya kuteremka daraja.





Manchester United wikiendi ijayo watapambana na Arsenal kwenye uwanja wa Emirates wakati wakisubiri kukabidhiwa kombe lao la ligi kuu katika mchezo wao mwisho kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Traford hapo May 12 watakapokuwa wakicheza na Swansea.



MSIMAMO WA  BARCLAYS PREMIER LEAGUE


NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
34
40
84
2
Man City
33
29
68
3
Arsenal
34
30
63
4
Chelsea
33
31
62
5
Tottenham
33
17
61
6
Everton
34
13
56
7
Liverpool
34
19
51
8
West Brom
33
-1
45
9
Swansea
33
1
42
10
West Ham
34
-7
42
11
Fulham
34
-8
40
12
Southampton
34
-7
39
13
Norwich
34
-20
38
14
Sunderland
34
-7
37
15
Stoke
34
-11
37
16
Newcastle
34
-17
37
17
Aston Villa
34
-27
34
18
Wigan
33
-23
31
19
QPR
34
-27
24
20
Reading
34
-28
24





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad