![]() |
|
Solar
Panels
Matumizi
ya nguvu za jua.
|
Benki
ya Dunia kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) zinatarajia
kusambaza umeme wa mionzi ya jua (SOLA) katika zahanati sita na shule sita za
sekondari katika vijijini vya Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kufunga Umeme Vijijini (RESCO),Bw. Mzumbe Mussa amesema hayo
jana(April 22,2013) alipokuwa akizungumzia shughuli zinazotarajiwa kutekelezwa
na kampuni yake kwenye zahanati na sekondari katika vijiji hivyo.
Alisema
hatua hiyo inalenga katika kuwaboreshea mazingira ya kuishi kwa watumishi wa
zahanati hizo.
Bw.Mussa
alisema lengo la msaada huo ni kuisaidia serikali kuboresha huduma kwa wananchi
wa vijijini wanaokabiliwa na changamoto za ukosefu wa nishati ya umeme.
Aidha
alieleza kwamba Benki ya Dunia imekuwa
ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini, kutatua baadhi ya
changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Zahanati
zitakazonufaika na msaada huo ni Kalenge, Nyakanazi, Ngalalambe, Katahoka,
Kasozibakaya na Mbindi.
Kwa
upande wa wa shule ni za Runazi na Nyantakara.






No comments:
Post a Comment