Fulham 0-1 Arsenal: goli la Mertesacker kwa kichwa na kuirejesha Arsenal nafasi ya 3 katika Msimamo wa Ligi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 21, 2013

Fulham 0-1 Arsenal: goli la Mertesacker kwa kichwa na kuirejesha Arsenal nafasi ya 3 katika Msimamo wa Ligi.

Arsenal
Arsenal wamerudi na kutwaa nafasi ya 3 baada ya kushinda huko Craven Cottage kwa kuitungua Fulham Bao 1-0 katika Mechi ambayo walisuasua licha ya kusaidiwa na Fulham kucheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 12 baada ya Steve Sidwell kupewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya aliyomfanyia Mikel Arteta.


Bao la ushindi kwa Arsenal lilifungwa na Per Mertesacker kwa kichwa katika Dakika ya 43.


Arsenal nao walimaliza Mechi hii kwa kuwa Mtu 10 baada ya Straika wao Olivier Giroud kupewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya.


Lakini matokeo mengine ya Mechi za leo ni balaa kwa Reading na QPR ambazo Jumatatu Usiku zitashushwa Daraja ikiwa Aston Villa itaifunga Manchester United Uwanjani Old Trafford.


Katika mchezo wao Reading, Timu ya mkiani, imekaribia zaidi kushuka Daraja baada ya kutandikwa Bao 2-1 na Norwich City ambao walipiga Bao zao 2 ndani ya Sekunde 90.



Jumamosi Aprili 20,2013.


Fulham 0 Arsenal 1



Norwich 2 Reading 1



QPR 0 Stoke 2



Sunderland 1 Everton 0



Swansea 0 Southampton 0



West Brom 1 Newcastle 1



West Ham 2 Wigan 0



MSIMAMO


NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
33
40
81
2
Man City
32
31
68
3
Arsenal
34
30
63
4
Chelsea
32
31
61
5
Tottenham
32
15
58
6
Everton
34
13
56
7
Liverpool
33
19
50


Jumapili Aprili 21,2013.


Saa 9 na Nusu Mchana


Tottenham v Man City


Saa 12 Jioni


Liverpool v Chelsea


Jumatatu Aprili 22,2013.


Saa 4 Usiku


Man United v Aston Villa


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad