Klabu ya
Azam FC imelazimishwa sare ya bila kufungana jioni hii(April 20,2013) na Klabu ya AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo
wa kwanza wa Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo
yanaifanya Azam FC iwe na mtihani mgumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili
zijazo Morocco, wakitakiwa lazima kushinda au kutoa sare ya mabao ili kufuzu.
Pamoja na
sare hiyo, Azam FC watakumbuka sana mabao matatu ya wazi
waliyokosa kupitia kwa washambuliaji wao wa pembeni, Kipre Herman Tchetche
mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja, Kipre
aligongesha mwamba mashuti mawili katika dakika za 51 pembeni kushoto
katikati na dakika ya 90+1 mwamba wa juu
katikati baada ya jitihada za kuwatoka mabeki wa AS FAR Rabat.
![]() |
| Azam FC |
Khamis Mcha
naye alimtoka vizuri beki wa pembeni wa AS FAR Rabat dakika ya 52 lakini
akapiga nje shuti lake.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Emile Fred wa Shelisheli, aliyesaidiwa na
nduguze Steve Maire na Jean Ernesta pembeni, kipindi cha kwanza Azam
walionekana kucheza kwa tahadhari zaidi na kufanya mashambulizi machache.
Lakini
kipindi cha pili, walifunguka na kuanza kushambulia moja kwa moja jambo ambalo
liliweka kwenye misukosuko lango la AS FAR Rabat kwa muda mrefu hadi wachezaji wa
timu hiyo kuanza kufanya hila za kupoteza muda ili kupunguza kasi ya wenyeji.







No comments:
Post a Comment