![]() |
|
Kamanda
wa Polisi Mkoa
wa Dodoma,
Kamishna
Msaidizi wa Polisi,
David Misime.
|
Mtoto wa
kike mwenye umri wa mwezi moja na nusu amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Mpwapwa akiwa amechanika vibaya sehemu zake za siri huku akipata haja kubwa na
ndogo kupitia sehemu moja.
Habari za
awali ambazo zilipatikana zilidaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na babu
yake mzaa baba.
Akizungumza
katika wodi namba saba ya hospitali hiyo mama mzazi wa mtoto huyo Regina
Msemakweli (24), mkazi wa Kijiji cha Isingu alisema kuwa mtoto wake alimzaa
Februari 25, mwaka huu akiwa njiani kuelekea hospitali kujifungua.
Alisema
kuwa, Aprili 17, mwaka huu alikwenda kisimani na kumuacha mtoto huyo akiwa na
mama mkwe na mtoto wake mwingine mdogo mwenye umri wa miaka miwili, lakini
aliporudi kutoka kisimani alimkuta mtoto wake akilia bila kunyamaza.
Regina
alisema kuwa baada ya kuona mtoto akilia bila kunyamaza aliamua kwenda
kumuogesha ndipo aligundua sehemu za siri za mtoto huyo zikiwa zimechanika
vibaya na alianza kutoa haja kubwa na ndogo kwenye sehemu ya haja ndogo.
Akizungumza
kwa uchungu alisema kuwa hakuwa ameelewa kimetokea nini kwani hata mama mkwe
wake hakusema kitu lakini madaktari baada ya kumchunguza mtoto walisema kuwa
amebakwa.
“Nasikia tu
na mimi kuwa watu wanasema amebakwa na baba mkwe wangu lakini wakati kitendo
hicho kinatokea nilikuwa kisimani,” alisema.
Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Dk Lunemo Sakafu alisema kuwa, mtoto huyo
alifikishwa hospitalini hapo na walipomchunguza waligundua kuwa alikuwa akitoka
haja kubwa na ndogo kwenye sehemu moja.
Daktari huyo
amesema kwamba hizo ni dalili za kuingiliwa kwa nguvu kwa binti huyo. Alisema
kuwa baada ya kufanya uchunguzi na kubainisha hayo walimwanzishia matibabu.
Hata hivyo
Muuguzi Mkunga wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Mary Mgonela alisema kuwa,
mtoto huyo na mama yake ambaye alisindikizwa na wifi yake alipokelewa katika
hospitali hiyo siku nne zilizopita.
Alipohojiwa
baba wa mtoto huyo yuko wapi alisema kwamba alikataa kwenda hospitalini kwa
madai kuwa alikuwa anakwenda kuchunga ng’ombe.
Alisema kuwa
baada ya kuonekana suala hilo ni gumu na lazima litolewe taarifa Polisi, wifi
wa mama huyo alielekezwa kwenda Polisi kuchukua PF 3 lakini alipotoka hakurudi
na wala Polisi hakufika.
Alisema kuwa
baada ya wifi huyo kutoonekana ilibidi ripoti itolewe kwa daktari na kisha
Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Alisema kuwa
katika maelezo ya mama wa mtoto kabla ya kufika hospitali walianza kwenda kwa
mganga wa kienyeji ambapo mganga huyo alimwambia kuwa hawezi suala hilo na
ndipo walipoamua kuja hospitali.
Muuguzi huyo
alisema kuwa, mtoto huyo ameumizwa vibaya na anaendelea kupatiwa matibabu huku
madaktari wakijitahidi wanavyoweza kuokoa maisha yake.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, David Misime alisema kuwa,
hana taarifa juu ya tukio hilo na atalifuatilia.






No comments:
Post a Comment