![]() |
|
Waziri
wa Afya Zanzibar,
Juma Duni Haji.
|
Waziri
wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji, ameshangazwa na wimbi la uuzaji wa dawa za
nguvu za kiume uliojitokeza katika maeneo ya misikiti visiwani humo.
Akifunga
mjadala kuhusu ripoti ya Kamati ya Maendelo na Ustawi wa Jamii, Wanawake na
Watoto ya mwaka 2012/2013 , Waziri Duni alisema waganga wamevamia maeneo ya
misikiti na kuuza dawa za kienyeji zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Alisema
inashangaza kuna dawa zinazouzwa na za wanaume pekee lakini akasema ni jukumu
la wananchi wenyewe kuwa makini kwa vile siyo kila daktari wa tiba asilia
anaweza kutibu kila aina ya maradhi.
Hata
hivyo,Waziri Duni alisema kwa upande
mwingine, vyombo vya habari vimekuwa vikichangia kuwaingiza wananchi katika
matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa ubora wake kutokana na kutangaza bila
kupata ukweli wa dawa hizo.
Alisema
baadhi ya dawa zinazouzwa huchangia matatizo ya wagonjwa kutokana na kuzitumia
bila maelekezo ya kitaalam, hivyo wanapozidiwa na kwenda hospitali, ugonjwa
huwa mkubwa na wengine kupoteza maisha.
Hata
hivyo, Duni alisema ataendelea kusimamia ukweli kwa vile umri wake unafikia
ukingoni.
Alisema
serikali imeshatunga Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira namba 11 ya mwaka
2012 ambayo itasaidia kuondoa matatizo ya matumizi mabaya ya tiba asilia.
Chanzo:
NIPASHE






No comments:
Post a Comment