![]() |
|
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wa tatu
kushoto) akiwa meza kuu na Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Kampuni yanayotoa
huduma za simu nchini.
|
Watumiaji,
watoa huduma, wakala wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwa ujumla
wamekumbushwa kuwa ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya
simu ambayo haijasajiliwa.
Akitoa tamko
la pamoja kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa
Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Prof. John Nkoma amesema ni kosa la jinai
kutumia namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki 5
au kifungo cha miezi mitatu.
Ameongeza
kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na
Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, mtu yeyote ambaye anauza au anatoa kwa namna
yeyote ile namba namba ya simu bila kuisajili anatenda kosa la jinai na adhabu
yake ni faini ya shilingi 3,000,000 au kifungo cha miezi 12 au vyote.
Aidha Prof.
Nkoma amewashauri watumiaji wa simu za mkononi na wananchi kuunga mkono juhudi
zinazofanywa ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na
kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta nay a Taifa kwa
ujumla.
![]() |
|
Baadhi
maafisa mbalimbali na wawakilishi wa makampuni yanayotoa huduma za simu nchini
katika mkutano huo.
|
![]() |
|
Sehemu ya
wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini.
|










No comments:
Post a Comment