Rais wa Jamhuri ya Kenya ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya kwakutangaza majina ya mawaziri wanne. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 23, 2013

Rais wa Jamhuri ya Kenya ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya kwakutangaza majina ya mawaziri wanne.


Rais Uhuru Kenyatta
Rais wa Jamhuri ya Kenya Bw.Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne.

 


Mawaziri hao wanne  ni pamoja na :-





Dkt. Fred Okeng'o Matiangi :- ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano.



Bw.Henery Rotich :- ameteuliwa wizara ya Fedha.



Bw. James Wanaina Macharia :- ndiye Waziri mteule wa Afya.



Balozi Amina Mohammed :- ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.





Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. 





Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja Mawaziri watakaoteuliwa na Rais.





 kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.





Chini ya katiba ya Kenya sharti Bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, Mabalozi  na Wakuu wa tume za Kikatiba.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad