![]() |
|
Mchoro
wa utumbo
wa
binadamu
|
Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo
sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni.
Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:
VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine’, vinaweza kuleta matatizo
kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo,
hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi.
Kimsingi
vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au
kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.
ULAJI CHUMVI
Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo.
Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula
vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi
nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani
wakati wa kula.
MAFUTA YA SAMAKI
MAFUTA YA SAMAKI
Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa.
Na
kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo
na magonjwa mengine ya tumbo.
VITAMINI NA MADINI
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika.
Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula
matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na
matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream
za maziwa huleta ahueni.
STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO
Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti.
Japo
msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya
tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza
kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya
ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha.
Vidonda Vya
Tumbo Ni Nini?
VIDONDA vya
tumbo ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha
ndani ya tumbo.
AINA ZA
VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya
tumbo vimegawanyika sehemu mbili; vidonda vya ndani ya tumbo (gastric ulcer) au
sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenal ulcer).
Vidonda
vinavyotokea katika utumbo ndivyo maarufu sana na huonekana zaidi kutokea kwa
wanaume, na vidonda vya ndani ya tumbo huwashambulia wote wanaume na wanawake.
Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja kati ya watu kumi
atakuwa na vidonda vya tumbo.
Vidonda vya
tumbo hutokeaje mwilini?
Chakula
kinapoingia tumboni kwa ajili ya kusagwa, tumbo huzalisha majimaji mbalimbali,
miongoni mwayo yaliyo muhimu zaidi ni asidi hidrokloriki.
Asidi hii
huanza kula kuta za tumbo/doudeni. Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea
kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo
katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.
Utokeaji wa
vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili.
Kwanza: vitu
ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua,
vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa na baadhi
ya dawa kama corticostisteroids, caffeine, reseprine, n.k.
Pili:
udhaifu wa ute au kuta za tumbo/duodeni kuzuia ushambuliaji wa asidi. Katika
kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kuongeza kinga ya ute au
kupunguza uzalishaji wa asidi.
Mfadhaiko wa
akili utokanao na shida za maisha.
Mfadhaiko wa
akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha
vidonda vya tumbo.
Mfadhaiko
huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo
hutiririka ndani ya tumbo imetengenezwa kwa ajili ya kukisaga chakula chochote
haraka iwezekanavyo.
Lakini kama
hakuna chakula cha kufanyiwa kazi, asidi hii humomonyoa kuta za tumbo na hivyo
kusababisha vidonda.
Utafiti
uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonesha kuwa akili hutumia biokemia
katika mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangakia sana katika
kutokeza kwa magonjwa mengi.
Utafiti wa
kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti
mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo
madhubuti au zilivyo dhaifu.
Ingawa
utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya
maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili/mawazo yatokanayo
na shida za maisha.
Majaribio
yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, wenye kupewa talaka na
wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa
mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.
Mfano katika
kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye
kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio,
msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya
maandalizi ya tendo.
Oksijeni na
virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe hadhiri zaidi,
na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni yenye nguvu huongezeka.
Kadiri
mfadhaiko unavyokuwa mfupi, ndivyo pia athari yake inavyokuwa fupi. Lakini
pindi mfadhaiko unapokuwa mrefu, kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au
katika hali ya matatizo, athari yake huendelea.
Dalili za
mfadhaiko.
Ikiwa bila
ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi
mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko.
Kujisikia
huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote, kupoteza kabisa uwezo wa
akili kufurahi, kupoteza hamu ya tendo la ngono na kupoteza hamu ya chakula (au
kula sana).
Nyingine ni
kukosa usingizi (au kulala sana), wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia pamoja,
kushindwa falakinika, kushindwa kukumbuka na kushindwa kuamua, kughadhibishwa
na vitu vidogo, kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.
Haraka
haraka
Haraka!
Haraka! Lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda
vya tumbo. Mbanano wa ratiba pia husababisha matumbo nayo kubanana.
Malalamishi
makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: "Tumbo langu linanisokota na
kuniletea matatizo, husikia kiungulia baada ya kula". Haraka na wasiwasi
ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.
Tumbo ni
kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia
hufungia breki kwenye viungo vya ndani.
Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa
mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli
na hapo husababisha kiungulia na maumivu.
Vyakula vya
kusisimua
Vyakula vya
kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa
vyakula vya kusisimua kama vile kachapu, haradali, achali, pilipili na vingine
vingi huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa
hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula
tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji huchoma. Tumbo linahitaji kupozwa na si
kusasuliwa.
Dalili za
vidonda vya tumbo
Vidonda vya
tumbo huambatana na maumivu ya kuchoma, kuwaka katika sehemu ya juu ya tumbo.
Kwa kuwa aina mbili zote za vidonda vya tumbo hutofautiana, ni vizuri zaidi
kuelezea kila kimoja.
(a) Vidonda
vya tumboni
Maumivu ya
vidonda vya tumboni mara nyingi hukaa katikati, takribani kati ya nusu ya chini
na kwenye kitovu na mara nyingi kula huifanya kuwa mbaya zaidi. Tofauti na
maumivu ya vidonda vya utumbo, maumivu ya vidonda vya tumbo mara nyingi
hayaishi mara moja pindi yanapoanza.
(b) Vidonda
katika utumbo
Maumivu ya
vidonda vya katika utumbo pia hukaa pale pale (kama katika vidonda vya
tumboni). Tofauti na vidonda vya tumboni, katika vidonda vya utumbo mara nyingi
kula husaidia kupunguza maumivu.
Tofauti
nyingine ni kuwa, wakati katika vidonda vya tumboni maumivu huongezeka haraka
baada ya kula chakula, katika vidonda vya utumbo inaweza kuchukua saa mbili au
tatu. Tabia nyingine ya vidonda vya utumbo ni kupotea kwa majuma au hata miezi
bila sababu ya wazi.
Mtu anaweza
kulalamika kuwa anapata maumivu baada ya chakula. Hii ni kutokana na msisimko
wa mnyunyizo wa asidi ambao hububujika kwenye kidonda. Katika vidonda vya
duodeni, huchukua takribani saa mbili hadi tatu ili asidi ifike sehemu ya
kidonda.
Utambuzi wa
vidonda vya tumbo
Utambuzi wa
kubainisha vidonda vya tumbo hujumuisha X-Ray. Upimaji wa tumbo na vilivyomo
ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama 'endoskopy' au
'biopsy', ambayo huyakinisha hali halisi.
Matibabu ya
vidonda vya tumbo
Matibabu ya vidonda
vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa
maalumu.
Ikiwa
matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo
upasuaji huwa muhimu.
Katika
vidonda vya tumbo ambavyo ni vikali, matibabu yake hutumia maziwa kwa mwanya wa
dakika 15 hadi saa mbili kwa kutegemea ukali wa ugonjwa; kwa wiki moja. Maziwa
hutumiwa pamoja na dawa.
Maziwa si
kwamba hupambana na asidi tu, bali pia huchelewesha muda wa tumbo kuruhusu dawa
kufanya kazi kwa muda mrefu. Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki
4-6 za matibabu.
Kuzuia
mfadhaiko
Kila mtu ana
matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara.
Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa
mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na
mfadhaiko ambao huweza kuwasabishia maradhi kama vidonda vya tumbo au maradhi
ya moyo, n.k.
Mfadhaiko
unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama
hautadhibitiwa.
Ni vipi
unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha?
(a)
Kuridhika na maisha
Kama
tutakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, tukaacha kuyakopa maisha ya jana
na tukaacha kuhofu maisha ya kesho, hakika kabisa matumbo yetu pia yatatulia.
Inaelezwa na
wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara duniani wanasumbuliwa na
maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na
wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa
wakiwa vijana.
Wasiwasi na
hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo
chanya katika kiwiliwili. Unaweza kuleta ugonjwa ambao ni wa kufisha kama ambao
hutokana na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari,
vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.
(b) Kutopata
usingizi wa kutosha
Ukosefu wa
usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za
dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa
maisha uko kila mahala. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya
watu ambao neva zao hazitulii.
Kulala ni
moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo,
udhaifu na uchovu.
Kukesha
usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na
pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na
akili.
Madaktari
wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole
kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya
makuzi ya afya njema ya mwili na akili.
Sehemu ya
kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na
asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa
athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya
kula.
Kiwango cha
wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka
miwili, mtu hushauriwa kulala saa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne saa 12-14
kwa siku, miaka sita hadi minane saa 11-12 kwa siku, miaka minane hadi 11 saa
10-11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 saa 8-9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa
za kulala kati ya sita na nane.
Elimu Na:Neemaherbalist






No comments:
Post a Comment