![]() |
| Anna Kibira |
Anna Kibira amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli nchini (CHANETA)
Katika uchaguzi uliofanyika jana (April 20,2013) Mkoani Dodoma.
Kibira
alikuwa Katibu Mkuu katika uongozi uliomaliza muda wake, lakini mwanzoni tu mwa
uongozi huo alisimamishwa kwa muda usiojulikana kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Katika
uchaguzi wa jana, Kibira alimuagusha Mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhanji.
Bhanji alikuwa Makamu Mwenyekiti katika uongozi uliomaliza muda wake.
Kibira
aliibuka na ushindi kwa kura 61 dhidi ya 21 za mpinzani wake huku Zainab Mbiro
ambaye mara kadhaa amekuwa akigombea lakini hachaguliwi, safari hii alibahatika
kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa
CHANETA.
Akitangaza
matokeo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Betty Mkwassa alisema, mpinzani
wa Mbiro Agnes Mangasila alipata kura 25 dhidi ya 57 za Mbiro.
Agness
Hatibu aliyekuwa peke yake kwenye nafasi ya Mweka Hazina, alipata kura 66 huku
kura 17 zilimkataa.
Wajumbe
walionekana kutaka sura mpya kwani waliwatosa wale waliokuwa kwenye uongozi
uliomaliza muda wake ambao ni Mary Protas, Mwajuma Kisengo na Rose Kisiwa na
kuwachagua Yasinta Silvester, Fortunata Kabeja, Asha Sapi, Penina Igwe, Hilder
Mwakatobe na Judith Ilunda katika nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Mapema kabla
ya uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi alitoa changamoto kwa
uongozi mpya CHANETA kuhakikisha wanaweka kanuni na viwango ili kuondokana na
migogoro isiyo ya lazima kwa ajili ya manufaa ya mchezo huo.






No comments:
Post a Comment