Sakata la Gesi ,Mkuu wa kaya ilipo gesi anusurika kutekwa, wananchi wachoma moto gari. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 25, 2013

Sakata la Gesi ,Mkuu wa kaya ilipo gesi anusurika kutekwa, wananchi wachoma moto gari.

Mkuu wa Kaya ya Msimbati ambako gesi asilia inachimbwa mkoani Mtwara, Bibi Somoe Mtiti (106) amenusurika ‘kutekwa’ na mtu anayeaminika na wakazi wa eneo hilo kuwa ni mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa baada ya wananchi kuvamia gari lake na kuliteketeza kwa moto jana usiku.

 

Hivi karibuni Bibi Mtiti aliionya Serikali juu ya mpango wake wa kusafirisha gesi ghafi kwenda Dar es Salaam kwa madai iwapo itapuuza onyo hilo bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi iliyokusudiwa.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki alisema hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa mhusika hajakwenda polisi kulalamika.


Kwa mujibu wa wanakijiji hao, mtu huyo ambaye ana asili ya kijiji hicho waliyemtambua (jina linahifadhiwa) aliwasili kijijini hapo jana saa 10 jioni akiwa na gari dogo aina ya Mark II na kwenda nyumbani kwa shangazi yake.


Habari zaidi soma:http://www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad