Kamanda wa
Polisi
Mkoa
wa Kagera,
Philip
Kalangi
|
Kundi la Majambazi
limeteka mabasi matano mojawapo likiwa
la wanajeshi wa Rwanda na kupora abiria na kisha kuwacharaza viboko.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,
Philip Kalangi amesema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi alfajiri katika Kijiji
cha Kikoma kilichoko Kata ya Rusahunga, Wilaya ya Biharamulo.
Mashuhuda wa
tukio hilo wameeleza kuwa majambazi hao
wakiwa na silaha za kivita, waliweka kizuizi na kuyasimamisha magari hayo moja
baada ya jingine kasha kuwashusha abiria
na kuwapora kila kitu walichokuwa nacho.
“Baada ya
kuwapora abiria, waliamua kuwacharaza viboko mmoja baada ya mwingine, kisha
kutokomea kusikojulikana,” alisema shuhuda mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina
lake liandikwe na kuongeza.
“Magari
yaliyotekwa ni Toyota Hiace, gari moja ni la wanajeshi waliokuwa wakitokea
Rwanda kwenda Dar es Salaam.”
Diwani wa
Kata ya Rusahunga,Bw. Amon Mizengo alisema tukio hilo lilihusisha majambazi
wanane waliokuwa na bunduki sita za kivita.
Diwani huyo
amesema magari yaliyotekwa yalikuwa yakitokea Ngara na Benaco na kuwa baada ya
abiria kuporwa kila kitu, waliamuriwa kuendelea na safari zao.
Kamanda
Kalangi amesema Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Eneo hilo
limekuwa likiripotiwa matukio kadhaa ya ujambazi na mwaka 2007 wabunge
wanaotokea maeneo hayo waliomba kuwekwa kwa minara ya mitandao ya simu ili kuwa
na mawasiliano.
No comments:
Post a Comment