Makalio yanaposababisha Video ya P-Unit inayojulikana kama "You Guy" Kupigwa Marufuku kuoneshwa na Television ya Citizen TV kisa kuonekana kwenda kinyume na maadili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 25, 2013

Makalio yanaposababisha Video ya P-Unit inayojulikana kama "You Guy" Kupigwa Marufuku kuoneshwa na Television ya Citizen TV kisa kuonekana kwenda kinyume na maadili.

Vera Sidika
Msichana anaesadikika kusababisha video ya kundi la  P-Unit itwayo "YOU GUY" kuzuiwa kuoneshwa na kituo cha Televisheni cha Citizen nchini Kenya, Vera Sidika (pichani) amezungumzia sakata hilo linaloendelea nchini humo.

 

Vera akilizungumzia suala hilo, anasema, "Ina maana Citizen TV hawaoneshi video za Rihanna akiwa nusu uchi, wanaonesha video nyingi za aina hii kutoka ughaibuni ambazo si nzuri.



Hata hivyo hiki ni kizazi kipya. Nilikuwa nimevaa gauni tu."




Vera alipoulizwa kuwa, anadhani video hii imezuiliwa kwa sababu yake, alijibu "Binafsi, sidhani kama kweli, labda ni kwa sababu ya mwili wangu ndo maana wanapindisha maneno, kama ingekuwa ni msichana mwembamba isingeonekana kuwa ni mbaya ila kwa sababu ya makalio yangu, watu ndiowanachanganyikiwa na hilo"



Mapema mwaka huu, Television ya Citizen TV iliifungia video ya P-Unit inayojulikana kama "You Guy" kutokana na kuonekana kwenda kinyume na maadili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad