Manchester United wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa Pointi 7 mbele , Chelsea kukamata nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu Uingereza kwa Mwaka 2012 ,sasa kwa Klabu zote Mechi zao za Ligi zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 31, 2012

Manchester United wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa Pointi 7 mbele , Chelsea kukamata nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu Uingereza kwa Mwaka 2012 ,sasa kwa Klabu zote Mechi zao za Ligi zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013.

Chelsea.
Frank Lampard, Miaka 34, ambae mwishoni mwa Msimu Mkataba wake unamalizika na inadaiwa tayari hana nafasi Klabu hapo, leo alivaa utepe wa Nahodha na kuibeba Chelsea toka Goli 1 nyuma Uwanjani Goodison Park na yeye mwenyewe kupiga Bao mbili na kuwapa ushindi wa Bao 2-1, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza kwa Miaka minne Uwanjani hapo.
Hi ilikuwa ni Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England kwa Mwaka 2012 kwa Klabu zote mbili ambazo zitacheza Mechi zao za Ligi zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013 kwa Chelsea kuikaribisha QPR Uwanjani Stamford Bridge na Everton kuwa ugenini huko St James Park kuivaa Newcastle.




Ushindi huu wa leo umeipaisha Chelsea kukamata nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City huku wao wakiwa na Mechi moja mkononi.

Liverpool.
Bao 3 ndani ya Dakika 28 za kwanza leo zimewapa Liverpool, waliocheza bila Meneja wao Brendan Rodgers ambae ni mgonjwa, ushindi wa 3-0 na kuzidi kuwadidimiza mkiani mwa Ligi Kuu England QPR huku Liverpool wakipanda nafasi moja na kumaliza Mwaka 2012 wakiwa nafasi ya 9.

Ushindi wa Liverpool ulipatikana kwa Bao za Luis Suarez, Bao 2, na Daniel Agger.
Theo Walcott.
Arsene Wenger amesema Hetitriki ya Theo Walcott aliyopiga jana Arsenal ilipoitwanga Newcastle 7-3 haina uzito wowote kwenye mustabali wake Klabuni hapo ambapo kuna mvutano huku Mchezaji huyo akigoma kukubali Mkataba mpya wakati Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa Msimu na kuanzia Januari Mosi yuko huru kuongea na Klabu nyingine zinazomtaka.

Wenger ametamka: “Nia yangu ni asaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji wa hapa na hata kama angecheza vibaya na Newcastle bado sisi tunataka aongeza Mkataba!”

Walcott, Miaka 23, amefunga Bao 14 Msimu huu na 4 ni katika Mechi 3 ambazo amechezeshwa kama Straika wa Kati.

Arsenal
Arsenal ilimsaini Walcott akiwa na Miaka 16 kutoka Southampton Mwaka 2006 kwa Dau la Pauni Milioni 5 ambalo lilipanda hadi Pauni Milioni 12.5.

Akiongea mara baada ya Mechi na Newcastle, Walcott alisema: “Mazungumzo na Arsenal yanaeendelea na nina hakika mambo yatakamilika hivi karibuni.”

Aidha mchezaji huyo Theo Walcott ameihakikishia Arsenal kumaliza Mwaka 2012 kwa mguu mzuri alipopiga Hetitriki na kutengeneza bao mbili zilizowabomoa Newcastle Bao 7-3 Uwanjani Emirates katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza.

Manchester United
Nao Manchester United watauanza Mwaka mpya 2013 wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa Pointi 7 mbele baada ya kuifunga West Bromwich Albion Bao 2-0 Uwanjani Old Trafford.

Bao la kwanza la Man United ni la kujifunga mwenyewe Gareth McAuley akijaribu kuokoa krosi ya Ashley Young.

Bao la Pili kwa Man United lilifungwa katika Dakika ya 90 na Robin van Persie, alietokea Benchi Kipindi cha Pili kumbadili Shinji Kagawa aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza tangu Oktoba kufuatia kuuguza Goti lake.

Manchester City
Wakicheza Mtu 10 Uwanjani Carrow Road kufuatia Kadi Nyekundu kwa Mchezaji wao Samir Nasri, Mabingwa watetezi Manchester City walisimama kidete na kuibuka washindi kwa Bao 4-3 dhidi ya Norwich City.

Man City walitangulia kwa Bao 2 mbele ndani ya Dakika 4 za kwanza mfungaji akiwa Edin Dzeko lakini Norwich wakapata Bao moja lililofungwa na Anthony Pilkington.

Licha ya kucheza Mtu 10 kufuatia kutolewa Nasri, City walipiga Bao la 3 kupitia Sergio Aguero na Russel Martin akaifungia Norwich Bao la pili na kuifanya Gemu iwe 3-2 lakini shuti la Dzeko liligonga mwamba na kumbabatiza Kipa Mark Bunn na kuipa City Bao la 4.

Bao la 3 kwa Norwich lilifungwa na Russell Martin.
Tottenham wao  wameshinda Mechi yao ya 6 kati ya 8 kwenye Ligi walipotoka nyuma kwa Bao la Nahodha wa Sunderland, John O’Shea, na kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Carlos Cuellar kujifunga mwenyewe na Winga Aaron Lennon kupiga Bao la pili na la ushindi.


Jumanne 1 Januari 2013


SAA 9 Dak 45 Mchana]


West Brom v Fulham


[SAA 12 Jioni]

Man City v Stoke

Swansea v Aston Villa

Tottenham v Reading

West Ham v Norwich

Wigan v Man United


[SAA 2 na Nusu Usiku]

Southampton v Arsenal



Jumatano 2 Januari 2013



[SAA 4 Dak 45 Usiku]


Chelsea v QPR

Liverpool v Sunderland



[SAA 5 Usiku]

Newcastle v Everton

+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:







1 Man United Mechi 20 Pointi 49



2 Man City Mechi 20 Pointi 42



3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38



4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36



5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]



6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]



7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]



8 Stoke Mechi 20 Pointi 29



9 Liverpool Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]



10 Swansea Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]





11 Norwich Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]



12 West Ham Mechi 19 Pointi 23



13 Sunderland Mechi 20 Pointi 22



14 Fulham Mechi 20 Pointi 21



15 Newcastle Mechi 20 Pointi 20



16 Wigan Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]



17 Aston Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]



18 Southampton Mechi 19 Pointi 17



19 Reading Mechi 20 Pointi 13



20 QPR Mechi 20 Pointi 10
 

1 comment:

Post Bottom Ad