Mbunge
wa Jimbo la Ubungo,
John
Mnyika.
|
Kwa mujibu
wa mtandao wa Bunge, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) ndiye anashikilia
rekodi ya ukinara wa kuchangia akifuatiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe
Zitto (CHADEMA) na Godfrey Zambi wa Mbozi Mashariki (CCM).
Utafiti huo
ambao hauhusishi takwimu za mkutano wa Novemba haukuwajumuisha mawaziri,
manaibu wao, Spika, naibu wake, wenyeviti watatu wa Bunge, Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile nafasi zao zinawapa
uwezekano mkubwa wa kuchangia hoja wakati wowote.
Katika
rekodi hiyo, Mnyika ambaye hiki ni kipindi chake cha kwanza bungeni, amechangia
mara 184, kuuliza maswali ya nyongeza 28 na ya msingi 7, Zitto amechangia 79,
maswali ya nyongeza 25 na maswali ya msingi 8, huku Zambi akiwa amechangia mara
70, maswali ya nyongeza 26 na ya msingi 9.
![]() |
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini,
Kabwe
Zitto.
|
Kulingana na
takwimu hizo, wabunge kumi waliochangia na kuuliza maswali mara chache ni
Mwanakhamis Said Kassim (CCM), ambaye rekodi inaonesha hajawahi kuuliza swali
la msingi wala nyongeza isipokuwa amechangia mara mbili tu.
Anayefuata
ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu mwaka 2008, Lowassa ambaye vile vile hajawahi
kuuliza swali la msingi wala nyongeza bali kachangia hoja mara mbili.
Katika kundi
hilo wamo Mbunge wa Rorya, Airo aliyechangia mara tatu, maswali ya msingi
matatu, wakati Muhammed Amour Chombo (CCM) hajawahi kuuliza swali bali
amechangia mara nne.
Muhammed
Seif Khatib (CCM), hajawahi kuuliza swali bali amechangia mara tatu huku Ali
Haji Juma (CCM), ameuliza swali moja la msingi, moja la nyongeza na kuchangia
mara nne.
![]() |
Mbunge wa
Monduli,
Edward
Lowassa.
|
Wamo pia
Anna Maulida Komu (CHADEMA) na Shwawana Bukhati Hassan (CCM) ambao wamechangia
mara tano bila kuuliza maswali wakati Meghji akiwa amechangia mara tisa bila
kuuliza swali.
Rekodi hiyo
pia inawaonesha Dk. Abdulla Juma Saadalla (CCM), Said Suleiman Said (CUF) na
Salim Hassan Turky (CCM) waliochangia mara saba, na kuuliza swali la nyongeza
moja.
Mbunge wa
Gairo, Ahmed Shabiby (CCM), ndiye anafunga orodha hiyo akiwa amechangia mara
tano na kuuliza swali moja la msingi na moja la nyongeza.
Katika kumi
bora ya wabunge waliochangia mara nyingi, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu (CHADEMA) anashika nafasi ya nne akiwa amechangia mara 93, ameuliza
maswali ya nyongeza 19 na msingi 7, akifuatiwa na Diana Chilolo wa Viti Maalumu
(CCM) aliyechangia mara 61, maswali ya nyongeza 41 na msingi 9.
Mbunge wa
Kawe,
Halima Mdee.
|
Nafasi ya
sita inashikiliwa na Halima Mdee wa Kawe (CHADEMA) akiwa na amechangia mara 59,
maswali ya nyongeza 15 na ya msingi 6 akifuatiwa na Moses Machali wa Kasulu
Mjini (NCCR-Mageuzi) mwenye michango 57, nyongeza 30 na maswali ya msingi 7.
Chritowaja
Mtinda (CHADEMA) amechangia mara 53 na kuuliza maswali ya msingi 12 na nyongeza
19 akifuatiwa na Magdalena Sakaya (CUF) aliyechangia mara 52, maswali ya
nyongeza 13 na ya msingi 4.
Mbunge wa
Kisarawe, Seleman Jafo (CCM) alifuatia kwa michango 51, maswali ya nyongeza.
Habari na:http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.
No comments:
Post a Comment